Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waliokuwa wajumbe wa kamati ya utekelezaji wa makubaliano iliyosainiwa tarehe 22,Agosti ,2019 kati ya jeshi la zimamoto na uokoaji na kampuni ya ROM Solutions Co.LTD leo Feb.5,2020 wamewasili ofisi za Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa [TAKUKURU]makao makuu jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kashfa ya kufanya mkataba mbovu wa Trilioni Moja bila kupitishwa na bunge.
Idadi ya wajumbe waliofika katika ofisi hizo leo ni sita ambapo walifika ofisi za TAKUKURU pamoja na kompyuta mpakato [Laptop]walizopewa na kampuni ya ROM SOLUTIONS CO.LTD.
Wajumbe hao pia walikuwa wakilipwa posho za vikao USD 800 na kampuni hiyo wakati wakiwa wanakutana katika vikao vyao vya majadiliano.
Wajumbe hao ni pamoja na Kamishna wa zimamoto Mbaraka Semwanza,Naibu Kamishna wa zimamoto Fikiri Salla,Naibu Kamishna wa Zimamoto Lusekelo Chaula’.
Wengine ni Naibu Kamishna zimamoto Ully Mburuko,Mchumi zimamoto Boniface Kipomela na Mchumi wa jeshi hilo la zimamoto na uokoaji Felis Mshana.
Ikumbukwe kuwa sakata hilo la mkataba mbovu wa Trilioni moja limesababisha aliyekuwa waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola kuachishwa wadhifa huo na kuteuliwa mwingine hivi karibu George Simbachawene.
Social Plugin