VIRUSI HATARI VYA CORONA VYATUA NIGERIA


Serikali ya mji wa Lagos nchini Nigeria imethibitisha kuwa, kesi ya kwanza ya maambukizi ya virusi vya korona (COVID-19) imeripotiwa katika mji huo wa kibiashara na wenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini humo.

Kamishna wa Afya wa mkoa wa Lagos, Akin Abayomi amesema, raia mmoja wa Italia aliingia nchini Nigeria jumanne kwa ziara ya kikazi akitokea Milan, na akaugua siku inayofuata. 

Amesema raia huyo alithibitishwa kuwa na virusi vya korona alhamis na taarifa kutolewa mara moja kwa Wizara ya Afya nchini humo.

Amesema mgonjwa huyo anaendelea vizuri na amelazwa kwenye Hospitali ya Magonjwa ya Kuambukiza iliyoko eneo la Yaba mjini Lagos. 

Pia amesema, wahudumu wa afya wanafanya jitihada kutambua watu wote waliowasiliana na mgonjwa huyo tangu alipowasili nchini Nigeria.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post