Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastani Kitandula ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Madini na Nishati katikati akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga kulia na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya REA Tanzania Julius Kalolo wakati wa ziara yao ya kufanya tathimini kuona wakandarasi wamefikia hatua gani mpaka sasa kwenye mradi huo wilayani Mkinga
Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastani Kitandula ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Madini na Nishati katikati akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga kushoto na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya REA Tanzania Julius Kalolo wakati wa ziara yao ya kufanya tathimini kuona wakandarasi wamefikia hatua gani mpaka sasa kwenye mradi huo wilayani Mkinga
Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastani Kitandula ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Madini na Nishati kushoto akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga kushoto wakati wa ziara yao ya kufanya tathimini kuona wakandarasi wamefikia hatua gani mpaka sasa kwenye mradi huo wilayani Mkinga kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya REA Tanzania Julius Kalolo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga kulia akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo
KAIMU Mkurugenzi wa Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga amewaonya wakandarasi wanaozembea katika utekelezaji wa miradi hiyo nchini kwa kutokukamilisha ndani ya muda uliopangwa la sivyo watachukuliwa hatua za kimkataba ikiwemo kuvunjiwa mikataba na kukatwa fedha.
Mhandisi Maganga aliyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani Mkinga alipotembelea vijiji vya Mbuyuni, Segoma, Sega na Mnyenzani ambapo pia walipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wakiwa wameambatana na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Nishati na Madini Dustan Kitandula.
Ambapo alisema madhumuni ya ziara hiyo ni kufanya tathimini kuona wakandarasi wamefikia hatua gani mpaka sasa wametembelea kwenye kazi walianzia Mkoani Manyara kijiji cha Terati leo wapo mkoa wa Tanga katika wilaya ya Mkinga.
Alisema kwamba madhumuni makubwa ya ziara yao ni kuona mradi wa Rea awamu ya tatu mzunguko wa kwanza ulianza mwaka Mwezi June 2018 na huo mradi ni wa
miaka miwili na sasa wamebakia miezi miwili au mitatu kumaliza mradi.
Alisema kwamba baada ya kutembelea mradi huo hawajaridhika sana na utendaji wake wa kazi wa mkandarasi wa Jarika na jinsi walivyoongea nae na aliwahaidi kufikia mwezi wanne atakuwa amemaliza hivyowananchi wa mkoa huo wawe na subira kati ya mwezi wa tatu au wa nne vijiji vyote ambavyo vinapaswa kupatiwa umeme vitakuwa vimenufaika.
“Labda niseme tu kwamba tutahakikisha wakandarasi wanaosimamia miradi huu wanakwenda kukamilisha ndani ya muda uliopangwa nawasipofanya hivyo taratibu za kimkataba zitachukuliwa kwanza watakatwa fedha tukiona
wanaendelea na mambo hayo hayo tutavunja mikataba “Alisema
“Pia niwaambie kwamba wakishindwa huo mradi wasitarajie watapata mradi mwengine watakuwa kwenye orodha ya wakandarasi ambao hawatapata kazi tena hivyo wakazane ili kuepukana na hali hiyo”Alisema Mhandisi Amon
Hata hivyo alisema aliwataka wakandarasi hayo kufanya kazi kwa bidii ili kampuni zao ziendelee kufanya kazi huku akieleza kwamba wao wanahitaji kufanya kazi na makapuni wazawa hivyo waonyeshe kwa vitendo uwajibikaji wao
katika kutekeleza miradi wanayokabidhiwa.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastani Kitandula alisema kwamba serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha inafanikisha zoezi la kupeleka umeme vijijini na kazi kubwa imefanyika
bahati nzuri yeye alishiriki kwenye jambo hilo tokea wanaanzisha Rea.
Alisema wakati Rea ikianzishwa walitenga fedha kutoka kwenye mafuta ya taa na mafuta mwengine ili ziende kutumika kutengeneza mradi huo ukiangalia
walipotokea na sasa serikali imefanyia kazi kubwa sana yapo mafanikio kutokana na kwamba kasi ya kupelekea umeme vijijini imekuwa kubwa sana.
Aidha alisema kwamba changamoto za REA awamu tatu ni katikati walipata tatizo la wakandarasi kupata vifaa nguzo ilikuwa ni tatizo huku uzalishaji kwenye viwanda vya nyaya napo kulikuwa na tatizo lakini sasa zimeondoka.
“Changamoto kubwa ni kwamba kwenye utekelezaji wa miradi bado kuna urukwaji wa maeneo unapelekea umeme kijiji x chenye vijiji vinne unakuta mkandasi ule wigo wa kufanyia kazi amepewa mdogo unakuta anapeleka kwenye vitongoji viwili vyengine vinabaki wamekuwa wakipigia kelele kila wakati”Alisema
Kitandula ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Madini na Nishati alisema kwamba ni matumaini yake awamu ya tatu ya REA mzunguko wa pili utaondoa hilo tatizo kwa wananchi.
Hata hivyo pia aligusia suala la ushirikishwaji viongozi kwenye maeneo husika ambapo aliwataka wakandarasi wapokwenda kwenye wilaya na vijiji wanavyotekeleza miradi huyo wahakikishe wanawashirikisha viongozi wa vijiji
na wilaya ili kuepka kuruka sehemu za huduma muhimu kama vile shuleni, nyumba za ibada na zahanati.
“Kwani wasiposhirikisha vuongozi hao matokea yake inasababisha sehemu za huduma muhimu kama vile Zahanati, nyumba za ibada na shule yanaacha kupatiwa umeme na hivyo kushindwa kunufaika na huduma hiyo muhimu”Alisema
Naye kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bwiti (CCM) Bakari Mkuya alishukuru kwa ujio wa Kaimu Mkurugenzi huyo kwenye wilaya hiyo huku akieleza kwamba changamoto zilizopo ni nyingi ambazo mbunge wao amejaribu kuzitatua.
Alisema kwamba kuna sehemu zina mapungufu miongoi mwa vijiji kuna maeneo mengine yamerukwa hasa vitongoji kwenye kata ambapo nguzo zimefika lakini kuna maeneo yameachwa hivyo wawasaidie kuwaambie wahakikishe wanayafikia
“Lakini tatizo kubwa ni kwamba kilio kikubwa baadhi ya nyumba vimerukwa tunamini hilo litafanyiwa kazi n mamlaka husika kuona namna kuondosha hali hii”Alisema Diwani huyo.
Social Plugin