Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAJESHI NA POLISI WAVAMIA BUNGE LA EL SALVADOR WAKITAKA MUSWADA WAO UPITISHWE


Wanajeshi na maafisa wa polisi waliojihami nchini El Salvador wamevamia bunge , wakitaka kuidhinishwa kwa mkopo wa dola milioni 109 ili kuwanunulia vifaa vya kukabiliana na uhalifu.


Waliingia katika jengo la bunge wakati rais Nayib Bukele alipokuwa anakaribia kuwahutubia wabunge .

Siku ya Ijumaa aliwapatia siku saba za kuunga mkono mpango wake wa kuchukua mkopo. Viongozi wa upinzani walitaja uvamizi huo wa wanajeshi bungeni kuwa kama kitendo cha kutishia.

Taifa la El salvador lina viwango vya juu vya mauaji duniani. Ghasia nyingi hutekelezwa na magenge ya uhalifu ambayo hufanya kazi katika eneo la Marekani ya kati.

Rais Bukele ambaye alichukua mamlaka mnamo mwezi Juni 2019 , anataka kutumia mkopo huo kuimarisha vifaa vya maafisa wa polisi na wanajeshi katika vita dhidi ya uhalifu.

Ameahidi kukabiliana na ghasia zinazotekelezwa na wahalifu pamoja na ufisadi katika taifa hilo lenye viwango vya juu vya umasikini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com