TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA WATUHUMIWA WANNE WA WIZI WA MABILIONI YA BENKI YA NBC JIJINI DSM
______________________
KUKAMATWA WATUHUMIWA WANNE WA WIZI WA MABILIONI YA BENKI YA NBC JIJINI DSM
______________________
Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia watu wanne waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya G4S Security kwa tuhuma za wizi wa Tsh 1.280,000,000/=,USD402,000 na Euro 27,700. Watuhumiwa hao ni;
1. CHRISTOPHER CLEOPHACE RUGEMALILA (34) dereva wa G4S, mkazi wa Chanika
2. MOHAMEDI ATHUMANI RAMADHANI (40) mlinzi G4S, mkazi wa mtoni kijichi
3. IBRAHIMU RAMADHANI MAUNGA (49), Mlinzi G4S, mkazi wa kiluvya.
4. SALIMU SHAMTE (45) mkazi wa Mbagala kizuiani.
Mnamo tarehe 07/02/2020 watuhumiwa watatu ambao ni
CHRISTOPHER RUGEMALILA, MOHAMEDI ATHUMANI na IBRAHIMU MAUNGA wakiwa na gari namba T 728 BAN, NISSAN HARD BODY, mali ya kampuni ya G4S, Gari la kusindikiza fedha.
Walinzi hao walikabidhiwa fedha kutoka tawi la benki ya NBC Kariakoo na NBC samora ili wazipeleke makao makuu ya benki ya NBC yaliyopo posta ya zamani sokoine drive, lakini hawakufanya hivyo, matokeo yake walipanga njama na kuelekea maeneo ya Temeke Maduka mawili karibu na kituo cha mafuta cha CAMEL na kuchukua fedha zote na kupakia kwenye gari ndogo T.134 DHY Toyota IST ikiendeshwa na SALUMU SHAMTE. Watuhumiwa hao baada ya kufanikisha uhalifu huo walitelekeza gari la Kampuni ya G4S, silaha mbili mali ya G4S, moja aina ya pump action, na bastola moja, mashine ya kuhesabia fedha na muhuri wa Benki ya CBA kisha kuondoka kusikojulikana.
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam baada ya kupata taarifa hizo liliunda kikosi kazi na kuanza ufuatiliaji mara moja, ambapo tarehe 17/02/2020 majira ya mchana huko Mongo la ndege Mtuhumiwa wa kwanza aitwaye CHRISTOPHER CLEOPHACE RUGEMALILA alikamatwa na alipopekuliwa alikutwa na Tsh 110,000,000/= USD 19,000 zikiwa ndani ya gari lake T 691 BMW DSU, Magari matano yenye namba za usajili, kama ifuatavyo;
- T691DSU BMW yenye thamani yake Tsh 15,000,000/=
- T909DSU Toyota Runx yenye thamani Tsh 13,000,000/=
- T627DSU Toyota IST yenye thamani ya Tsh 11,000,000/=
- T653DSU Toyota IST, yenye thamani ya Tsh 11,000,000/=
- T857DSU Toyota IST. yenye thamani ya Tsh 11,000,000/=
Mtuhumiwa baada ya kuendelea kuhojiwa alikiri tayari ameshanunua nyumba mbili na kiwanja kimoja vyenye thamani ya TSH 107,000,000/= samani za ndani vyenye thamani ya Tsh 5,000,000/= na kufanya jumla ya mali na fedha taslimu Tsh 297,110,000/= USD 21,000.
Tarehe 21/02/202 watuhumiwa wawili walikamatwa MOHAMED RAMADHANI na SALIMU SHAMTE huko Mbagala na walipopekuliwa walikutwa na Tsh 332,000,000/= USD 50,000, EURO 5010 na GARI T134 DHY Toyota IST iliyotumika kubebea fedha baada ya kuiba na kutelekeza gari la kampuni ya G4S.
Watuhumiwa wote wawili baada ya mahojiano walikiri kununua viwanja viwanja viwili maeneo ya kisemvule na kivule vyenye thamani ya Tsh 25,000,000/=. Jumla kuu ya mali na fedha taslimu ni Tsh 357,000,000/= USD 50,000 na EURO 5010
Aidha upelelezi uliendelea na tarehe 24/02/2020 mtuhumiwa IBRAHIMU RAMADHANI MAUNGA alikamatwa na baada ya kupekuliwa alikutwa na Tsh 195,213,450, USD 70,600, nyumba aliyonunua kibaha Tsh 30,000,000/= na samani za ndani zenye thamani ya Tsh 10,000,000/=
Jumla kuu ya mali na fedha ni Tsh 253,000,000/=
Jeshi la polisi kanda maalum limefanikiwa kukamata watuhumiwa wote watatu pamoja na mtuhumiwa mmoja ambaye aliwasaidia kukamilisha wizi huo.
Sambamba na hilo, tunawashikilia askari Polisi tisa kwa kukiuka maadili ya kazi wakati wa ufutiliaji na upekuzi wa tukio
hili.
KUUWAWA KWA JAMBAZI SUGU JIJINI DSM
Katika tukio la pili, mnamo tarehe 24/02/2020 majira ya saa saba na nusu usiku huko maeneo ya saba saba mbagala kizuiani, kikosi kazi cha kupambana na majambazi kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa RAMADHANI RASHIDI @ASNEY MJEURI (20) mkazi wa mbagala, mtuhumiwa huyo wakati mahojiano alikiri kujihusisha na tuhuma mbalimbali za ujambazi maeneo ya TOANGOMA, Mbagala na Mkuranga. Ndipo alikubali kwenda kuwaonyesha askari alipoficha silaha na watuhumiwa anaoshirikiana nao na walipofika eneo hilo alianza kukimbia huku akipiga kelele na askari walifyatua risasi tatu hewani kumuamuru asimame lakini mtuhumiwa huyo aliendelea kukimbia na ndipo alipopigwa risasi mgongoni na kufariki dunia.
LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
25/02/2020
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
25/02/2020
Social Plugin