Vibanda zaidi ya 30 vya wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga wapatao 200 vimeteketekea kwa moto ulioanza majira ya saa 10 usiku katika eneo la Makoroboi jirani na msikiti wa Wahindi jijini Mwanza.
Vyanzo vya habari vinaeleza kwamba moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme na uunganishaji holela wa nyaya za umeme,mali mbalimbali za machinga hao zimeteketea kabisa na hakuna mtu yeyote aliyepata madhara kutokana na moto huo.
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Nyamagana Daktari Philis Nyimbi amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa zoezi la kubainisha vibanda vingine vilivyoteketea linaendelea.
Social Plugin