Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania -TEC unatangaza taarifa za Vifo vya watumishi 5 wa TRC.Vifo hivyo vimesababishwa na ajali ya Treni ya uokoaji kugongana na Kiberenge No.HDT-3 katika maeneo yaliyopo kati ya stesheni za Mwakinyumbi na Gendagenda tarehe 22.3.2020.
Eneo hili lipo katika Reli inayotoka Ruvu Junction mpaka Mruanzi Junction.
Watumishi wa TRC walikua sita, Watumishi wanne wamefariki pale pale katika eneo la ajari na majeruhi wawili walifikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya(magunga) Korogwe kwa huduma za Kitabibu.
Mpaka ilipofikia saa tano usiku (23:00) tarehe 22.3.2020 majeruhi mmoja alifariki na kufikia jumla ya watumishi wa TRC watano wamefariki.
Watumishi hao ni :
1.Ramadhani Gumbo-DTM Tanga
2.Eng.Fabiola Moshi DME DSM
3.Joseph Komba - ATM DSM
4.Philip Kajuna -Safety Technical
5.George Urio - Dereva wa trolley
Mpaka sasa majeruhi mmoja anaendelea na matibabu ni Guard wa treni Elizabeth Bona.
Poleni sana familia ya Reli kwa tukio hili la kusikitisha sana.
Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusu maandalizi ya kuhifadhi miili ya wapendwa wetu.
Aidha uchunguzi wa kujumuisha taasisi zingine utafanywa kubaini chanzo cha ajali hii mbaya.
Bwana ametwaa na Bwana ametoa, Jina lake lihidimiwe🙏🙏
Social Plugin