.
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Innocent Bachungwa (aliyenyanyua mkono) akiangalia mashine za kukamua mafuta kwenye kiwanda cha Mt. Meru mjini Singida;
kiwanda kinachosadikiwa kuwa kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki na Kati, mbele yake ni Mkuu
wa Wilaya ya Singida, Injinia
Paskasi Muragili nyuma yake ni
Sailesh Patel, Makamo wa Rais wa Kiwanda cha MT Meru-Tanzania
Na John Mapepele, Singida
Waziri wa Viwanda na
Biashara, Innocent Bichungwa ameitaka Wizara yake kwa kushirikiana na Mkoa wa
Singida ndani ya mwezi moja kufanya
mkutano wa kitaifa utakaowashirikisha wadau wote wa zao la Alizeti.
Mkutano huo utakuwa ni wa kujadili
mnyororo wa thamani wa zao hili
kuanzia kwa mkulima hadi kwa wenye
viwanda ili kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kufuta gharama kubwa
ambazo serikali inatumia kuagiza mafuta ya kula toka nje ya nchi.
Bachungwa ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya
siku mmoja leo kwenye Mkoa wa Singida
kutembelea viwanda vya kukamua Alizeti ambapo alikagua shughuli zinazofanywa na
kiwanda kikubwa cha kukamua mafuta
Afrika mashariki na Kati cha Mt. Meru na
Kiwanda cha Singida Fresh Mill vilivyopo
ndani ya Manispaa ya Mji wa Singida.
Alisema lazima kuwepo na mkutano huo haraka wa wadau
wote wa zao hilo ili kunusuru fedha
nyingi zinatumika na nchi kununua mafuta ya kula kutoka nje ya nchi
Alisema katika kundi la
bidhaa la vyakula, mafuta ya kula yanashika nafasi ya pili kuwa kutumia gharama
ya asilimia 22.6 ikiongozwa na zao la Ngano
linalotumia asilimia 57.3 huku Sukari
ikitumia asilimia 16.2 ikifuatiwa
na Mahindi ambayo yanatumia gharama ya asilimia
2.6 kulipiwa toka nje ya nchi ambapo aliongeza kuwa Tanzania kama nchi inatumia jumla ya
kiasi cha shilingi trioni 1.3 kwa mwaka
kuagiza bidhaa zote za vyakula
kutoka nje ya nchi.
Bachungwa alisema
Tanzania imejaliwa kuwa na maeneo makubwa
ya ardhi yenye rutuba ambayo yanaweza kupanda
mbegu bora za Alizeti ambazo zinaweza kutosheleza viwanda vya ndani na
kuuzwa nje ya nchi, kinachotakiwa ni wadau wote kukaa kama taifa na kujadii namna bora ya kuongeza thamani kwenye
mnyororo wa mzima wa thamani wa zao la Alizeti.
Aliwataja baadhi ya wadau
muhimu katika kikao hicho kuwa mikoa inayolima zao la Alizeti, wizara inayohusika
na kilimo, Mifugo na Uvuvi, Fedha, tasisi za utafiti zinazojiusisha na Alizeti,
wajasiliamali na wawekezaji wa viwanda
vikubwa vya kukamua mafuta ya Alizeti hapa nchini.
Alisema alichogundua katika
ziara hiyo ni kuwa hakuna mfumo mzuri wa kufungamanisha kilimo cha alizeti na viwanda hali inayowafanya wadau washindwe kupata faida na badala yake kuhangaika kutafuta
masoko ya bidhaa hizo nje ya nchi na
kuwakosesha watanzania ajira na mapato
kwa taifa.
“Nimeshangaa viwanda
vinahangaika kuuza mashudu nchi jirani na kulalamikia kodi na ushuru unaotozwa
na Serikali wakati tunaviwanda vyetu vya kutengeneza vyakula vya kuku
vinahangaika usiku na mchana kutafuta
mashudu wakati Singida yamejaa”
alihoji Bachungwa
Aliutaka Mkoa wa
Singida kutumia fursa ya kuwa jirani na Makao Makuu ya Nchi,
Dodoma kupanga mipango mizuri kwa
kutenga maeneo maalum ya uwekezaji kama
ambavyo Mkoa wa Pwani ulivyonufaika kwa kuwa
karibu na Jiji la Dar es Salaam
kwa kutenga maeneo ambayo sasa
maeneo hayo yameendelea kujengwa
viwanda vya kisasa hivyo kuendana na
kauli ya Serikali ya awamu ya
Tano inayosisitiza ujenzi wa viwanda
Aidha aliwataka watendaji
Serikalini kote nchini kubadilika na
kuondokana na dhana kwamba mapinduzi ya viwanda yataletwa na Wizara ya Viwanda na Biashara na badala yake mikoa
iweke mikakati mahususi ya
kuwavutia wa wekezaji kuja kuwekeza na
baada ya kuwekeza waendelee kuwalea
ili waweze kuendelea kuweka mitaji
zaidi ktika mikoa husika.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt. Rehema Nchimbi alimshukuru
Waziri Bachungwa kwa kufanya ziara hiyo ambapo alisema tayari mkoa wake umeshafanya vikao vya mara kwa mara na wadau mbalimbali wa zao la
alizeti ambapo amesema hata wiki moja iliyopita Mkoa wa kushirikiana na Shirika
na Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Viwanda Vidogo Nchini (SIDO) walitoa
mafunzo maalum kwa wajasiliamali wa zao
hilo ambapo amesema mkutano huu utakuwa na manufaa makubwa kwa kuwa utakuwa
katika ngazi ya kitaifa na itashirikisha wadau wengi zaidi.
“Mkoa tunafarijika
sana kwa wazo lako ulilotoa la kuwa na
mkutano wa kitaifa wa wadau wote wa zao la Alizeti kwa kuwa ni ndoto yetu kuboresha thamani ya zao
hili ili kuleta mapinduzi makubwa kwa wadau wote na taifa kwa ujumla, nakuahidi
sisi kama Mkoa tutafanya haraka
iwezekanavyo kuhakikisha mkutano unafanyika ndani ya mwezi huu” alisisitiza
Dkt. Nchimbi
Alisema katika kuratibu
mkutano huo mkoa utawashirikisha wadau mbalimbali ambao wataandaa maonyesho
maalum ya mnyororo wa zao la Alizeti ili
washiriki waweze fursa kuona bidhaa
mbalimbali zitokanazo na zao hilo.
Aliongeza kuwa Mkoa umekuwa
ukifanya kampeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na kampeni ya mbegu hasara na
mbegu bora iliyolenga kuwafanya wakulima
kuachana na mbegu za asilia ambazo mavuno yake yalikuwa yanazidiwa mara saba zaidi na mbegu bora ya kisasa.
Alizitaja baadhi ya faida
ya mbegu bora kuwa ni kuokoa akiba ya
ardhi, kuokoa muda, bei ya kuuza kuwa
juu ambapo pia aliishukuru benki ya
kilimo nchini TADB kwa kutoa mikopo ya zaidi ya
bilioni 4 kwa wadau mbalimbali wa zao la alizeti kwenye mkoa wa Singida.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida Injinia
Paskasi Muragili ameishukuru
Serikali kwa kupanga kufanya mkutano huo kwenye Wilaya yake ambapo alisema Wilaya yake ndiyo
mzalishaji mkuu wa mbegu bora za Alizeti hivyo mkutano huo
utasaidia kuwapa msukumo mpya wadau wote kuboresha thamani ya mnyororo
mzima wa thamani wa zao hilo.
Social Plugin