Chama cha Likud cha Israel kinachoongozwa na waziri mkuu Bw. Benjamin Netanyahu kimepata viti vingi kwenye uchaguzi wa bunge, lakini takwimu zinaonyesha kuwa hakikupata viti vya kutosha kuunda serikali.
Takwimu zinaonyesha kuwa Bw. Netanyahu na vyama washirika vyenye mrengo wa kulia wa uyahudi wa kihafidhina wamepata viti 60, idadi ambayo ni pungufu kwa kiti kimoja kuunda serikali ya pamoja yenye viti 120.
Kundi la vyama vya mrengo wa kati-kushoto linaloongozwa na Bw. Benny Gantz limepata viti kati ya 52-54, chama cha Likud kinachoongozwa na Bw. Netanyahu kinatarajiwa kupata viti takriban 37, na mpinzani wake wakuu chama cha "Blue and White" kinachoongozwa na Benny Gantz kimepata viti takriban 33.
Wakati huohuo, katibu mkuu wa Ofisi ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) Bw. Saeb Erekat amelaani uchaguzi wa Israel unaotazamiwa kuwa ni kitendo cha "kuweka makazi, kutwaa na kuleta mgawanyo".
Social Plugin