Mgonjwa wa virusi vya corona nchini Tanzania amefariki dunia leo Jumanne Machi 31, 2020.
Taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu imethibitisha kifo hicho na kubainisha kuwa alikuwa akipatiwa matibabu katika kituo cha matibabu ya wagonjwa wa Covid-19 kilichopo Mloganzila.
"Marehemu ni Mtanzania mwanaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine.Tunamuomba Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, na tunatoa pole kwa familia, ndugu jamaa wa marehemu, " amesema Ummy.
Social Plugin