Vurugu na kurushiana maneno vimeibuka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakati wa kusikiliza kesi ya viongozi wa Chadema.
Hayo yote ni baada ya polisi kujaribi kuzuia baadhi ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuingia katika chemba za mahakama hiyo kwa ajili ya kusubiri hukumu ya viongozi wa chama hicho.
Polisi walilazimika kuwazuia wafuasi hao kwa maelezo, kwamba chumba cha mahakama hiyo kimejaa kutokana na watu kuwa wengi.
Kutokana na wafuasi wa Chadema kutokuwa tayari, lakini pia kujiridhisha kwamba nafasi ya kutosha ipo, waliendelea kuwa na msimamo wa kutaka kuingia ndani.
Kutokana na mvutano huo, polisi walilazimika kuruhusu baadhi ya wafuasi hao kuingia huku wengine wakibaki nje.
Leo tarehe 10 Machi 2020, mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya uchochezi Na. 112/2018 inayowakabili viongozi wa Chadema.
==>>Tazama hapo chini
==>>Tazama hapo chini