Na Faustine Gimu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesitisha tamko lake la kufanya mikutano ya hadhara kote nchini kutokana na ugonjwa wa Corona.
Mikutano hiyo iliyotangazwa kufanyika kuanzia April 04 mwaka huu imesitishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mh.Freeman Mbowe hii leo jijini Dodoma.
Akizungumza leo Machi 23, 2020, Jijini Dodoma, Mbowe amesema kuwa wakati anatoa kauli yake ya kutangaza uwepo wa mikutano ya hadhara kwa nchi nzima, Serikali haikuwa imetangaza uwepo wa mgonjwa yeyote wa Virusi vya Corona na kwamba wataendelea na mikutano yao pale ambapo hali ya ugonjwa huo itakuwa imetengemaa.
Aidha Mbowe ameiomba Serikali ione ipo haja ya kufunga mipaka yake yote ili kuhakikisha hakuna mgeni yoyote anayeingia nchini kutoka kwenye Mataifa yaliyoathirika na Virusi vya Corona.
Wakati huo huo Chama hicho kimetoa salamau za pole kwa familia kufatia kifo cha aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa kazi na ajira kabla ya kuhama Chama cha Mapinduzi na kuhamia CHADEMA ambako alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Ilala Dkt.Makongoro Mahanga
Social Plugin