Kisa cha kwanza cha virusi vya corona chathibitishwa Kenya. Wizara ya afya imethibitisha kisa hicho kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe.
Akizungumza na vyombo vya habari waziri huyo amesema kwamba kisa hicho kilithibitisha Alhamisi usiku.
Waziri huyo amesema kwamba kisa hicho ni cha kwanza kuripotiwa nchini Kenya tangu kuzuka kwa mlipuko huo mjini Wuhan nchini China.
Kisa hicho ni cha raia wa Kenya aliyewasili humu nchini kutoka Marekani kupitia mji London nchini Uingereza tarehe 5 mwezi Machi 2020.
Aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya wizara ya afya nchini Kenya.
Hathivyo waziri huyo amesema kwamba mgonjwa huyo ambaye ni mwanamke yuko katika hali njema na kwamba viwnago vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida.
''Tarahe 5 mwezi Machi aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya serikali lakini sasa viwango vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida anakula vizuri lakini hawezi kutolewa hadi virusi hivyo vitakapokwisha mwilini.''
Waziri huyo amewataka Wakenya kuwa watulivu na kuwacha wasiwasi.
Amesema kwamba serikali ya Kenya kupitia wizara ya afya itaendelea kuimarisha mikakati ili kuhakikisha kwamba hakuna usambazaji wa virusi hivyo zaidi.
Chanzo- BBC
Social Plugin