Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema watu 12 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona nchini Tanzania.
Katika hotuba yake kwa Taifa kiongozi mkuu huyo wa nchi leo Jumapili Machi 22, 2020 amebainisha kuwa kuanzia kesho Jumatatu Machi 23,2020 wasafiri watakaoingia Tanzania kutoka nchi zenye maambukizi ya corona watawekwa katika eneo maalum kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe.
“Mpaka sasa nchi yetu imebaini wagonjwa 12 ambao wamethibitika kuambukizwa corona. Kati yao wanne ni raia wa nje na wanane ni raia wa Tanzania. Wagonjwa wote isipokuwa mmoja ametoka kwenye nchi zilizokuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.”
“Kuanzia kesho Machi 23 wasafiri wote watakaoingia nchini kutoka kwenye mataifa yaliyoathirika zaidi na ugonjwa huu watalazimika kufikia sehemu zilizotengwa na kukaa huko kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe”,amesema Rais Magufuli.
Social Plugin