Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAJIBU YA MASWALI 10 YANAYOULIZWA SANA KUHUSU VIRUSI VYA CORONA

Mchakato wa ukuaji wa coronavirus hadi kufikia uwezo wa kusababisha ugonjwa huchukua siku 14, linasema Shirika la Afya Duniani (WHO)
Zaidi ya nchi 110 hadi sasa zimeripoti visa vya coronavirus na Shirika la Afya Duniani limetangaza virusi hivyo kuwa janga.

Yafuatayo ni majibu ya baadhi ya maswali ambayo wasomaji wamekua wakiyauliza.
1. Je inachukua kipindi gani mpaka mtu afahamike kuwa na coronavirus? - Swali lililoulizwa na Gillian Gibs
Inachukua siku tano kwa wastani kuanza kuonesha dalili, tangu mtu apate maambukizi, wanasayansi wamesema, lakini baadhi ya watu huanza kuonesha dalili hata baadae kuliko kipindi hiki.
Mchakato wa ukuaji wa coronavirus hadi kufikia uwezo wa kusababisha ugonjwa huchukua siku 14, Shirika la Afya Duniani (WHO), linasema. Lakini baadhi ya watafiti wanasema kipindi hicho kinaweza kuchukua hadi siku 24.
Kufahamu na kuelewa kipindi cha ukuaji ni muhimu sana. Huwasaidia madaktari na mamlaka za afya kuanzisha njia bora za kudhibiti usambaaji wa virusi.
2. Je ukipona coronavirus ina maanisha unakinga ? RubyRed aliuliza kwenye ukurasa wa Twitter.
Kusema ukweli ni vigumu kuelezea. Virusi hivi vimekuwepo tu tangu mwezi Disemba, lakini kutokana na uzoefu wa virusi vingine na coronaviruses unatakiwa kuwa na kinga ya mwili yenye uwezo wa kukabiliana na virusi ambayo itakulinda.
Mwanamke akikohoa

Kwa virusi vya Sars na virusi vingine vya aina ya coronavirus tulishuhudia maambukiuzi. Sasa kuna ripoti kutoka Uchina za watu ambao wanaruhusiwa kutoka hospitalini ambao walipatikana na virusi lakini hawakuwa na uhakika juu ya vipimo hivyo.

Hata hivyo, kitu muhimu ilikuwa ni watu hao hawakuwa na maambukizi tena.
3. Kuna tofauti gani kati ya coronavirus na mafua? - Brent Starr, Gresham, na Oregon, waliuliza kutoka Marekani.
Coronavirus na mafua ni maambukizi yenye dalili sawa jambo linalofanya utambuzi wake kuwa mgumu bila kufanyiwa kipimo.
Dalili ya kuangalia kupanda kwa joto la mwili na kikohozi. Mara kwa mara mafua huwa na dalili sawa na hizo pia, kama vile kuvimba koo, huku watu wenye virusi vya corona wakihisi kuishiwa na pumzi.
Watu ambao hufikiria kuwa huenda wameathiriwa na coronavirus wanahitaji kupata ushauri zaidi wa haraka wa kimatibabu.
Chati inayoonyesha dalili za coronavirus
4. Je kujitenga binafsi inamaanisha mtu afanye nini ? - Anauliza Alan Gel
Kujitenga binafsi inamaanisha mtu kukaa nyumbani kwa siku 14, sio kwenda kazini, shule au maeneo ya umma, na kuepuka kusafiri katika usafiri wa umma au teksi. Unapaswa pia kukaa mbali na wengine nyumbani kwako.
Omba msaada kama unahitaji huduma ziwe za chakula au matibabu , lakini hupaswi kumkaribisha mgeni yeyote,
5. Je corona ni hatari kwa watu wenye maradhi ya pumu? - Wameuliza Lesley-Anne, Falkirk
Maambukizi yatokanayo na mfumo wa hewa, kama vile coronavirus, yanaweza kusababisha mtu kuwa na dalili za pumu /asthma.
Wataalamu wa tiba ya ugonjwa wa pumu wanashauri watu wanaohofia virusi kufuata hatua za kudhibiti maradhi ya pumu.
Hii ni pamoja na kutumia vifaa maalumu vya kufungua njia ya hewa -inhaler kila siku kama inavyoshauriwa. Hii inasaidia kupunguza hatari za shambulio la pumu linaloweza kusababishwa na kirusi chochote cha mfumo wa kupumu, mkiwemo coronavirus.
Mwanamke akipiga chafya huku akiwa amejifunika pua na mdomo kwa kitambaa

6. Je coronavirus inaweza kuambukizwa kwa kufungua vitasa vya milango na vinaweza kuishi kwa muda gani? - Ameuliza Jean Jimenez

Kama mtu ameambukizwa kikohozi na kukoholea viganjani mwake na kugusa kitu fulani sehemu ya juu ya kitu hicho hua imeambukizwa.
Kitasa cha mlango ni mfano mzuri wa vitu ambavyo vinaweza kusababisha athari ya maambukizi ya coronavirus.
Wataalamu wanafikiria kuwa coronavirus inaweza kuishi kwenye eneo fulani huenda kwa siku kadhaa. Kwa hiyo ni bora kuosha mikono yako mara kwa mara ili kupunguza hatari ya maambukizi na kuenea kwa virusi.
7. Je ni salama kuogelea kwenye vidimbwi vya maji vya umma /Swimming pools? - Ameuliza Annette
Maji katika vidimbwi vingi vya kuogelea vya Umma huwa yana Chlorine, kemikali ambayo inaweza kuua virusi. Kwa hivyo kama inawekwa basi maji hayo yanapaswa kuwa salama kutumia vidimbwi vya kuogelea vya umma kwani huwa vinawekwa kemikali hiyo.
Hata hivyo, unaweza kupata virusi kutoka kwa mtu mwingine ambaye ameambukizwa hasa mnapokutana katika chumba cha kubadilisha nguo au kama jengo lina maambukizi kama vile kweye vitasa vya milango.
Na mtu fulani ana maambukizi ya virusi anaweza kuvisambaza kwa wengine kupitia kikohozi na chafya kama watagusana.
Kuna njia nyingi za kukusaidia kuepuka kupata au kusambaza maambukizi ya virusi.
Njia za kuzuia maambukizi
8Je ninapaswa kuanza kuvaa barakoa ili kupunguza uwezekano wa kueneza na kupata virusi? -Swali la Ann Hardman
Ingawa madaktari na wapasuaji mara kwa mara huvaa barako, kuna ushahidi mdogo sana kwamba uvaaji wa barakoa unaleta tofauti.
Mfano Idara ya afya kwa Umma nchini Uingereza imesema kuwa "haitoi ushauri matumizi ya barakoa kama njia ya kujilinda dhidi ya virusi".
Wataalamu wanasema usafi wa kutosha - kama vile kunawa mara kwa mara mikono yako na kabla ya kugusa uso wako-ni jambo la maana zaidi katika kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.
9Kuna hatari gani kwa watoto ? - Swali la Louise,
Kwa ujumla watoto wanaonekana kutoambukizwa sana coronavirus, kwa mujibu wa data kutoka China.
Hii huenda ikawa ni kwasababu wana uwezo wa kukabiliana na maambukizi au hawana dalili yoyote , au wanakua na dalili ndogo sawa na zile za mafua. Hatahivyo, watoto wenye matatizo ya mapafu, kama vile maradhi ya pumu, wanapaswa kuwa makini , kwani virusi vinaweza kusababisha shambulio la pumu.
Kwa watoto walio wengi, inaweza kuwa ni maambukizi ya mfumo wa kupumua kama mengine na hakuna sababu ya kuwa na hofu.
Watoto
11. Je unaweza kupata virusi kutoka kwenye chakula kilichoandaliwa na watu walio na coronavirus? - Aliuliza Sean
Mtu ambaye ameambukizwa coronavirus anaweza kusambaza virusi kwa mtu mwingine kama chakula walichoandaa hakikuandaliwa kwa usafi.
Virusi vinaweza kusambazwa kwa matone ya kikohozi yanayoanguka kwenye kiganja au mkono.
Kunawa mikono kabla ya kugusa au kula chakula ni ushauri mzuri kwa kila mtu katika kuzuia kusambaa kwa virusi.
CHANZO- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com