Mamlaka Ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imeadhimisha Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) leo Machi 9,2020 kwa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga juu ya haki za watumiaji wa Huduma za Mawasiliano.
Akizungumza, Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo alisema TCRA Kanda ya Ziwa imeadhimisha siku hii leo Machi 9,2020 ambapo Kidunia itafanyika Machi 15,2020 kwa kauli mbiu ya mwaka 2020, “The Sustainable Consumer” yaani Mtumiaji Endelevu.
Alisema mwamko wa utumiaji wa huduma na bidhaa endelevu unaendelea kuongezeka duniani kote hasa kwa watumiaji/walaji vijana. hivyo ni jukumu la Mamlaka ya Mawasilano Tanzania pamoja na watoa huduma wote kufanya watumiaji wa bidhaa na huduma waweze kufanya machaguo sahihi wa bidhaa wanazotaka.
“Watoaji wa huduma za mawasiliano nchini, wakiongozwa vyema na Mamlaka ya Mawasiliano wamekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia kuwa sekta hii ya mawasiliano inagusa Watanzania zaidi ya milioni 40 wanaotumia huduma mbalimbali kupitia simu zao za mkononi kama vile kupiga na kupokea simu, SMS, Intaneti na huduma za kifedha”,alisema Mhandisi Mihayo.
Alidha alisema watoa huduma wanatakiwa kumlinda mteja dhidi ya uhalifuwa kupitia huduma za kifedha kupitia simu za mkononi (Safeguard against mobile money fraud) kwa kuhakikisha taarifa zake za miamala ya kifedha hazidukuliwi.
“Mamlaka ya Mawasiliano itaendelea kusimimia watoa huduma watoa kwa kufuata sharia na kanuni zilizopo ili kuboresha mazingira ya utoaji huduma za Mawasiano hapa nchini”,aliongeza Mhandisi Mihayo.
Alibainisha kuwa Mamalaka ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa ndiye mwenye wajibu wa kuhakikisha huduma zinazotolewa katika mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Kagera na Geita ni bora na za uhakika.
“Vile vile ni jukumu letu kuhakikisha tunatoa elimu kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano kwa shirikiana na watoa huduma wa Makampuni ya simu ili kila mtumiaji atambue haki yake katika kutumia huduma ya mawasiliano na namna ya kuepuka uhalifu mitandaoni”,alisema Mhandisi Mihayo.
Naye Meneja
wa Tigo mkoa wa Shinyanga Sadock Phares akisoma Hotuba ya Mkurugenzi wa Kanda
ya Ziwa kutoka TIGO,Uthman Madati kwa niaba ya Umoja wa Makampuni ya Simu
Tanzania (TAMNOA), alieleza changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni utapeli katika huduma za kifedha
ambapo wateja wengi wamekuwa wakilalamika
kutapeliwa kwa njia moja au nyingine.
“Kama
mwakilishi wa Kampuni za mawasiliano tumetoa tahadhari ya changamoto hii katika
mawasiliano ambazo wengi wamekuwa wakikutana nazo hasa katika utapeli.Njia
mojawapo wa kupunguza ni kumsaidia mtumiaji kuelewa namna ya kuongeza umakini
katika matumizi ya mawasiliano hasa huduma za kifedha”,alieleza.
“Watoa
huduma tumeendelea kutoa elimu kwa umma na kuwasisitiza watumiaji wa huduma za
kifedha kwa njia ya simu kuhakikisha wanafahamu chanzo cha maombi ya pesa kwa
njia ya mtandao na kuhakiki watu wanaowatumia fedha kabla ya kutuma pesa ili
kupunguza au kuzuia athari za utapeli”,aliongeza Phares.
Aliitaja
changamoto nyingine ni kuwa Mteja kuwa na laini ya simu ambayo haikusajiliwa
kwa jina lake na kutoa taarifa ya uongo au maelezo yasiyo sahihi wakati wa
kusajili laini ya simu.
Maadhimisho
ya Siku ya Haki za Watumiaji Duniani,kwa kifupi WCRD yalianza 1983 kupitia shirika
la kimataifa lisilo la kiserikali la Consumer International (CI) na kukubalika
kuwa na maadhimisho kila tarehe 15 mwezi Machi ya kila mwaka na leo Mamlaka Ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imeadhimisha Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu haki za watumiaji wa Huduma za Mawasiliano. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano kutoka TCRA, Walter Mariki kutoka Makao Makuu ya TCRA akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano kutoka TCRA, Walter Mariki kutoka Makao Makuu ya TCRAakizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Tigo mkoa wa Shinyanga Sadock Phares akimwakilisha Mkurugenzi wa Kanda ya Ziwa kutoka TIGO,Uthman Madati kwa niaba ya Umoja wa Makampuni ya Simu Tanzania (TAMNOA),akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Tigo mkoa wa Shinyanga Sadock Phares akimwakilisha Mkurugenzi wa Kanda ya Ziwa kutoka TIGO,Uthman Madati kwa niaba ya Umoja wa Makampuni ya Simu Tanzania (TAMNOA),akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga.
Wanafunzi wa Chuo cha VETA wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga
Mratibu wa Mafunzo Chuo cha VETA, Rashid Hamis akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga
Wanafunzi wa Chuo cha VETA wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga.
Wanafunzi wa Chuo cha VETA wakisoma vitabu vya TCRA kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga.
Wanafunzi wa Chuo cha VETA wakisoma vitabu vya TCRA kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.