Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

IRAN YAKATA MSAADA WA MAREKANI


Kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei amesema Iran haitopokea msaada wowote kutoka Marekani, katika kubadili hali ilivyo kutokana na wimbi la maambukizi ya virusi vya corona nchini mwake. 

Katika taarifa yake hiyo Khamenei alirejea kuizungumzia dhana ya kwamba virusi hivyo ni silaha iliyoundwa na Marekani dhidi ya maadui zake.

Katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja kupitia televisheni kiongozi huyo amesikika akisema wana maadui wengi lakini, mkubwa kuliko wote ni Marekani.. na sasa anataka kuwasaidia. Ni vyema taifa hilo likajikita katika kuwasaidia wananchi wake. 

Iran limekuwa eneo tete la usambaaji wa virusi vya corona, ambavyo vilianzia China mwishoni mwa mwaka uliopita. 

Hata hivyo usambaaji wa visa hivyo ulianza kuingia Marekani wiki iliyopita. 

Marekani inakabiliwa na mamia ya vifo vyenye kuhusishwa na virusi hivyo, wakati Iran vifo vyake vinapindukia watu 1000. 

Katika hatua hiyo ya kukataa msaada, Khamenei aligusia nadharia ya kwamba virusi hivyo viliundwa na Marekani kwa lengo la kuyadhoofisha mataifa adui kama China na Iran. 

-DW


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com