Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JESHI LA POLISI MWANZA LAWATIA MBARONI WATU 6 KWA KUKUTWA NA ZANA HARAMU ZA UVUVI ..PIA LINAWACHUNGUZA POLISI KWA KUKIUKA MAADILI

Jeshi la polisi mkoa wa mwanza linawashikilia jumla ya watu sita kwa makosa ya kupatikana na zana haramu za uvuvi na kupatikana na dawa za kulevya (mirungi na bhangi).

Pia linachunguza kama kulikuwa na ukiukwaji Wa maadili ya kazi wakati wa ukamataji wa Watuhumiwa hao.

Tukio la kwanza jeshi la polisi mkoa wa mwanza limekuwa likifuatilia taarifa mbalimbali na kuzifanyia kazi kwa lengo la kuzuia uhalifu .

Tarehe 05.03.2020 huko maeneo ya bwiru Wilayani ilemela, jeshi la polisi mkoa wa mwanza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama Liliwakamata na linawashikilia watu watatu ambao jeremiah asam,@ amolo, miaka 48, mjaluo, Mfanyabiashara, mkazi wa bwiru – ilemela na wake zake wawili ambao ni joyce jeremiah, miaka 40, mjaluo, mkazi wa bwiru-ilemela na getruda david, miaka 26, msukuma, mfanyabiashara, mkazi wa nyasaka, kwa kosa la kupatikana na zana haramu za uvuvi ambazo ni nyavu(gillnet) 7,401, timba (monofilament) 178, nyavu za dagaa 3 Na kokoro la dagaa roller 1, katika makazi yake

Maeneo ya bwiru –ilemela na dukani kwake maeneo yaliberty –nyamagana. Hata hivyo baada ya watuhumiwa hao kukamatwa, yalijitokeza madai yaliyowalenga baadhi ya askari polisi kuwa wanadaiwa kukiuka maadili ya utendaji wa kazi.

Uchunguzi juu ya madai hayo unafanywa kwa kufuata mfumo wa kijeshi na ikibainika hatua za kinidhamu za kijeshi zitachukuliwa.

Tukio la pili, kukamatwa kwa msafirishaji na muuzaji maarufu wa madawa ya kulevya aina ya mirungi. Jeshi la polisi linamshikilia na linatarajia kumfikisha mahakamani mtuhumiwa peter charles mwita @ peter mirungi, miaka 46, mkurya, mkazi wa mtaa wa rufiji, kwa makosa ya kusafirisha, kusambaza na kuuza mirungi jijini mwanza.

Hata hivyo mtuhumiwa baada ya kujua anafuatiliwa na polisi tarehe 01.02.2020 alitelekeza gari namba t.787 dqx aina ya probox maeneo ya igoma mashariki, likiwa na Mirungi kiasi cha kilogramu 9.02. Aidha tarehe 15.02. 2020 mtuhumiwa tajwa hapo juu alikamatwa.

Amekuwa akifanya biashara hiyo haramu kwa muda na mkono wa dola sasa umemuangukia kwa hatua zaidi za kisheria.

Tukio la tatu tarehe 02/03/2020 majira ya 06:00asubuhi huko katika kizuizi cha magari kilichopo kijiji cha ngashe, kata ya lugeye, Wilaya magu, mkoa wa mwanza, askari wakiwa doria walikamata bhangi kiasi cha kilogramu 50, zikiwa katika magunia matatu, iliyokuwa ndani ya gari lenye namba za usajili t.881 afx na tela namba t.822 czz lori aina ya scania iliyokuwa ikitokea tarime kuja mwanza, iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina la joseph achiyo ambaye aliruka kwenye gari na kukimbia wakati gari liliposimamishwa na askari.

Jeshi la polisi mkoa wa mwanza linaendelea na msako wa kuhakikisha mtuhumiwa anatiwa nguvuni. Gari limekamatwa lipo kituoni.

Tukio la nne tarehe 02.03.2020 majira ya 16:30hrs jioni huko maeneo ya nyakato sokoni, wilaya ya nyamagana jiji na mkoa wa mwanza, askari wakiwa kwenye misako na doria waliwakamata faustine koroso, miaka 46, mkurya, mkazi Wa nyakato mashariki na gidion paul, miaka 28, Msukuma, mkazi wa igoma, wakiwa wanasafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kiasi cha kilogramu 20, kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili mc.931 ckl aina ya honlg, kitendo ambacho ni kosa la jinai.

Jeshi la polisi linaendelea na mahojiano na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Jeshi la polisi mkoa wa mwanza linaendelea kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo sheria. Vilevile jeshi la polisi mkoa wa mwanza linawataka askari wake kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za
Kazi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com