Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu, Salum Mwalimu na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche wametoka gereza la Segerea leo.
Mpaka sasa viongozi wote wa Chadema wametolewa jela isipokuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye mpaka sasa bado yuko gerezani.
Viongozi wengine wa Chadema ambao wameachiwa ni wabunge Halima Mdee (Kawe), Esther Bulaya (Bunda Mjini), Esther Matiko (Tarime Mjini) na Peter Msigwa (Iringa Mjini).
Chama hicho kimechangisha fedha kutoka kwa wanachama wake na watu wengine ambao wameguswa na hukumu ya viongozi hao ambao walihukumiwa kifungo cha miezi 5 jela au kulipa faini ya Milioni 350.
Social Plugin