Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akimsikiliza Mkurugenzi wa utafiti ,mafunzo na ugani kutoka wizara ya Mifugo na uvuvi Dkt.Angello Mwillawa kabla ya kuingia kufungua kikao cha baraza la saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo[LITA] lililofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na washiriki wa kikao wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo(LITA) lililofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo(LITA) lililofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo(LITA) lililofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa baraza kuu la wafanyakazi wa wakala wa vyuo vya mafunzo ya Mifugo[LITA]Dkt.Pius Mwambene,akizungumza kwenye kikao cha Baraza la saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo(LITA) kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa utafiti ,mafunzo na ugani kutoka wizara ya Mifugo na uvuvi Dkt.Angello Mwillawa,akizungumza kwenye kikao cha Baraza la saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo(LITA) kilichofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua kikao cha Baraza la saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo(LITA) lililofanyika jijini Dodoma.
........................................................................................................................
Na.Mwaandishi wetu,Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka Watumishi wa baraza kuu la wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) kuwa chachu katika kutatua changamoto za wafugaji.
Prof.Gabriel amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha baraza la saba la wafanyakazi la wa wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo[LITA] ambapo amesema watumishi wa sekta ya Mifugo ni moja ya chachu kubwa katika kutatua changamoto za mfugaji hapa nchini.
“Ninyi ni fursa muhimu sana katika kushauri program na kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya mifugo,hivyo baraza ndio chimbuko la fikra kwa kuleta mapinduzi makubwa katika sekta hii ya mifugo na kuwa chachu muhimu zaidi kutatua changamoto za mifugo hapa nchini”amesema Prof.Gabriel.
Aidha,Prof.Gabriel amesema watumishi katika sekta ya Mifugo walio na ngazi ya astashahada[cheti] na Stashahada [Diploma]wamekuwa wakifanya bidii katika kuwahudumia wafugaji ikilinganishwa na watumishi wenye ngazi ya Shahada[Degree] kwani baadhi ya watumishi wenye elimu ya juu wamekuwa wakijiona wako hadhi ya juu kumhudumia mfugaji wa kawaida ,hivyo wakati umefika kwa watumishi bila kujali elimu waliyo nayo kubadilika na kuwa karibu katika kumhudumia mwananchi wa kawaida.
Katika hatua nyingine Prof.Gabriel amesema changamoto inaweza kuwa fursa hivyo amewataka wafugaji na watanzania kwa ujumla kuhakikisha kuwa na desturi ya kugharamia na kuhudhuria kozi ya muda mfupi namna ya ufugaji bora ili kuwa na ufugaji wenye tija.
“Nakumbuka sitosahau nilipofiwa na baba yangu alikuwa mchungaji,tulinunua jeneza kwa laki nne,wakati mimi nalia nimepoteza mzee yangu lakini muuza jeneza ananiambia karibu tena majeneza yapo ,wakati nalia kwa uchungu muuza jeneza anasheherekea biashara imeenda vizuri ,maana yake ni kuwa changamoto inaweza kutengeneza fursa hivyo wafugaji ukijinyima kidogo ulichonacho ili upate mafunzo ya kozi fupi za ufugaji unaweza ukafikiri unapoteza fedha lakini hii utakuwa unajitengenezea mazingira mazuri ya kufuga mifugo watakaokueletea faida kubwa”amesema .
Pia Prof.Gabriel amelitaka baraza hilo kuona namna ya kuondoa utegemezi kutoka serikali kuu na huku akiitaka LITA kuwa na mahusiano mazuri zaidi na vyombo vya habari katika kujitangaza kwani vina mchango mkubwa katika kuinua uchumi kuelekea Tanzania ya viwanda.
Awali Mwenyekiti wa baraza kuu la wafanyakazi wa wakala wa vyuo vya mafunzo ya Mifugo[LITA]Dkt.Pius Mwambene amesema kuna changamoto mbalimbali hasa za miundombinu pamoja na upungufu wa wakufunzi takribani 34 wa afya ya mifugo huku juhudi zikifanyika ikiwa ni pamoja na ukarabati wa miundombinu na kubuni biashara ,mafunzo ya muda mfupi kwa wafugaji katika kukabiliana na changamoto hizo.
Naye Mkurugenzi wa utafiti ,mafunzo na ugani kutoka wizara ya Mifugo na uvuvi Dkt.Angello Mwillawa amesema tafiti zimekuwa na mchango mkubwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya sekta ya mifugo kwani husaidia katika kuweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza.
Wakala wa LITA ulianzishwa Tarehe 1/9/2011 kwa sheria ya wakala wa serikali Na.30 ya mwaka 1997 na marejeo yake ya mwaka 2007 ambapo kuanzishwa kwa wakala hiyo kulihusisha vyuo vya mifugo na kubadilishwa kuwa Campus kwa Muundo wa NACTE ambapo hadi sasa LITA ina jumla ya Watumishi 224 na Campus zote nchini zikiwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 2700 kwa wakati mmoja na mwaka huu wanafunzi 3634 Wamedahiliwa na kuwa na ziada ya wanafunzi 934 sawa na ongezeko la asilimia 34.6%.
Social Plugin