Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi William Lukuvi amemaliza rasmi ulaji uliokuwa unafanywa na baadhi ya maafisa ardhi wa jiji la Arusha.
Waziri Lukuvi amesema hayo mkoani Arusha tarehe 8/3/2020 wakati wa ziara yake ya kuanzisha rasmi ofisi za ardhi za mikoa na kuvunja ofisi za kanda ambazo zilikuwa zinahudumia zaidi ya mkoa mmoja, hali iliyokuwa inawasababishia wananchi usumbufu.
Akizungumza na viongozi wa mkoa huo wakati akianzisha rasmi ofisi mpya ya kanda ya mkoa wa Arusha amesema kuanzia sasa ulaji uliokuwa unafanyika na baadhi ya maafisa aridhi wa jiji kwa kudai posho za kwenda kufuatilia hati mkoa wa kilimanjaro ameaumaliza rasmi.
Ameongeza kuwa Huduma zote za utoaji hati, uandaaji wa michoro ya mipango miji, pamoja na huduma za Msajili wa Hati zitatolewa Katika Jiji la Arusha na sio katika makao makuu ya kanda Moshi kama ilivyokuwa hapo awali.
Hadi sasa Waziri Lukuvi ameishafungua ofisi za ardhi ngazi ya mkoa katika mikoa ya Singida, Tabora, Geita, Mara na Arusha na kazi inaendelea katika mikoa mingine yote nchini ambapo huduma zote za uandaaji na utoaji hati kuanzia sasa zinafanyika mkoani.
Hatua hii ya kuanzisha ofisi za ardhi ngazi ya mkoa imekuja ili kupunguza kero za wananchi kufuata huduma hiyo Wizarani au katika Makao makuu ya Ofisi za Kanda za mikoa mitatumitatu.