Maambukizi ya virusi vya corona nchini Afrika ya Kusini yameongezeka na kufikia watu 402, ikilinganishwa na watu 128 siku moja kabla na kulifanya taifa hilo kuwa lenye kiwango kikubwa zaidi cha maambukizi barani Afrika.
Rais Cyrill Ramaphosa ametangaza siku 21 za wananchi wote kujifungia ndani ilikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo
Ramaphose amesema wakati wa mpango huo ambao unatarajiwa kumalizika Aprili 16 hakuna mtu ataruhusiwa kutokana nyumbani na watakosimamia jambo hilo ni idara ya maafa ya nchi hiyo.
Amesema katazo hilo la watu kutoka ndani halitawahusu watu wa idara ya majanga, polisi na watumishi wa afya ambao watakuwa wakiwazungukiwa wananchi kuwapatia mahitaji muhimu ambayo ni pamoja na chakula.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na wizara ya afya zaidi ya nusu ya visa vilivyotokea Afrika Kusini vimepatikana katika jimbo la Gauteng, linalolijumisha jiji la Johannesburg, ambalo ni kubwa kabisa nchini humo lenye idadi ya watu milioni 5.7, na mji mkuu Pretoria ambao una watu milioni 2.4.
Afrika Kusini sasa inaipiku Misri kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ingawa bado hakujaripotiwa kifo.
Idadi kubwa ya visa vya maambukizi vinawahusisha wasafiri kutoka Ulaya na mataifa mengine, ingawa idadi ya maambukizi ya ndani pia inaongezeka.
Social Plugin