Mkuu wa Wilaya (DC) ya Dodoma Mjini nchini Tanzania Patrobas Katambi ameagiza mabasi yote yanayoingia jijini humo kupuliziwa dawa za kuua wadudu ikiwa ni hatua ya kukakibiliana na virusi vya Corona.
Akizungumza jana Ijumaa Machi 27 2020, Katambi amewaagiza Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Dodoma Mjini na halmashauri ya jiji kuhakikisha mabasi yote yanayokwenda mikoani kupigwa dawa ya kuuwa wadudu kabla na baada ya safari.
Ameagiza pia kupigwa dawa kwa maeneo yote yenye mikusanyiko mikubwa ya watu.
Amewataka wakazi wa Dodoma kufuata masharti yaliyotolewa na wataalam wa afya ili kuepukana na ugonjwa huo.
Social Plugin