NA FARIDA SAIDY,MOROGORO
Mvua zinazonyesha mkoani Morogoro zimeendelea kuleta madhara, ambapo baadhi ya Madaraja yamesombwa na maji na kufanya baadhi ya mitaa kutofikika, Mito mikubwa kufurika ukiwemo Mto Morogoro na Mto Mkundi iliyokatiza katikati ya Mji hivyo maji kutiririka kuelekea katika makazi ya watu.
Hata hivyo Wakazi waliopembezoni mwa mito hii mikubwa ukiwemo Mto Morogoro na Mto Mkundi wanasema, pamoja na hali hii kusababishwa na Mvua kubwa zinazo endelea kunyesha, Dalili za Mmomonyoko zilionekana wazi hata kabla ya msimu wa Mvua.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Mhandisi Mnene James wamesema hatua za uchunguzi zinaendelea, mpango ni kuchukua hatua za haraka kurejesha mawasiliano katika maeneo hatarishi.
Pamoja na uharibifu wa Miundombinu, imesha ripotiwa baadhi ya watu kupoteza maisha msisitizo ni wananchi kuchukua tahadhari hasa waishio mabondeni na wale wa pembezoni mwa mito Mikubwa.