Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad(CCM) ametoa msaada wa vifaa vya kazi ‘Aproni’ zenye thamani ya shilingi Milioni 2.4 kwa wajasiriamali 300 wanaojihusisha na uuzaji vyakula ‘Mama Lishe’ mkoa wa Shinyanga.
Mhe. Azza amekabidhi taulo hizo leo Jumapili Machi 8,2020 wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambapo katika mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Iselamagazi kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mhe. Azza amesema ‘Aproni’ hizo zitawasaidia Mama Lishe katika masuala ya kuboresha usafi kwa Mama Lishe katika maeneo yao kazi.
“Leo tukiwa tunaadhimisha siku ya wanawake duniani,natumia fursa hii kuwakumbuka wanawake wajasiriamali wanaofanya biashara ya chakula ‘Mama Lishe’ kwa kuwapatia ‘Aproni’ 300 zenye thamani ya shilingi Milioni 2 na laki nne ambazo zitagawiwa kwa wanawake 50 katika kila halmashauri ya wilaya mkoani Shinyanga”,alisema Azza.
Mbunge huyo aliwaomba Wakurugenzi 6 wa Halmashauri za wilaya kuzigawa Aproni hizo kwa usawa kwa wanawake wanaouza vyakula ‘Mama Lishe’.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad(CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya kazi ‘ Aproni’ zenye thamani ya shilingi Milioni 2.4 kwa wajasiriamali 300 wanaojihusisha na uuzaji vyakula ‘ Mama Lishe’ mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Machi 8,2020 kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambapo katika mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Iselamagazi kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya pamoja na baadhi ya Mama Lishe katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga baada ya kuwakabidhi vifaa vya kazi 'Aproni'.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Aproni 50 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika halmashauri hiyo.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Aproni 50 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Neema Mkanga kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika halmashauri hiyo.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Aproni 50 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Prisca Musoma kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika halmashauri hiyo.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Aproni 50 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu, Verena Peter Ntulo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika halmashauri hiyo.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Aproni 50 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kahama, Ashura Hoja kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika halmashauri hiyo.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Aproni 50 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu, Rehema Edson kwa ajili ya wanawake wajasiriamali katika halmashauri hiyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya kumbukumbu na Wakurugenzi/Wawakilishi wa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya 6 za mkoa wa Shinyanga waliopokea Aproni na watakwenda kuzigawa kwa Mama Lishe waliopo katika halmashauri zao.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya pamoja na baadhi ya Mama Lishe katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga baada ya kuwakabidhi vifaa vya kazi Aproni.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin