MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA) YATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA KWA MIKOA 19


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza angalizo la mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo katika mikoa 19 nchini humo kuanzia leo Jumanne Machi 3, 2020.


Taarifa ya TMA imeitaja mikoa hiyo ni; Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe, Pwani pamoja na visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba visiwani Zanzibar.

Imesema athari zinazoweza kujitokeza baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Taarifa hiyo imesema kesho Jumatano Machi 4, 2020 angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Iringa, Njombe, Tanga, Morogoro, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani pamoja na visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

Alhamisi ya Machi 5, 2020 mvua hizo zinatarajia kunyesha kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Iringa, Njombe, Tanga, Morogoro, Dar es Salaam, Pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
أحدث أقدم