Marekani imefanya mashambulizi ya anga dhidi ya wapiganaji wa Taliban Jumatano Machi 4, katika jimbo la Helmand, Kusini mwa Afghanistan, msemaji wa vikosi vya Marekani ametangaza.
Ni mashambulizi ya kwanza ya Marekani tangu Washington na Taliban kutia saini makubaliano ya kuondoka kwa vikosi vya nchi hiyo nchini Afhganistan siku ya Jumamosi wiki iliyopita.
Kanali Sonny Leggett, msemaji wa vikosi vya Marekani nchini Afghanistan, amethibitisha mashamulizi hayo kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Amesema wapiganaji wa Taliban "walishambulia kwa nguvu kizuizi cha barabara [cha vikosi vya usalama vya Afghanistan]. Mashambulizi tuliyotekeleza ni ya kujihami ili kukomesha shambulio hilo la taliban. "
Mkataba uliotiwa saini Jumamosi huko Doha, unaitaka Marekani kuondoa vikosi vyake ndani ya kipindi cha miezi 14 na serikali ya Kabul na Taliban kuanza mazungumzo.
Mashambulizi hayo ya kujihami ya Marekani yanajibu mashambulizi ya Taliban yaliyotokea usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano. Karibu askari 20 wa Afghanistan na polisi waliuawa.
-RFI
Social Plugin