Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBOWE ALIPA FAINI YA MILIONI 70, KUTOKA GEREZANI LEO MCHANA


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amelipa faini ya 70,000,000 na muda wowote leo Ijumaa Machi 13, 2020 atatoka katika gereza la Segerea.

Mbowe  ni kati ya viongozi wanane wa Chadema ambao pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji Jumanne Machi 10, 2020 walihukumiwa kulipa faini ya Sh350 milioni au kwenda jela miezi mitano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 12 kati ya 13 yaliyokuwa yanawakabili. 

Yeye alihukumiwa kulipa faini ya sh. milioni 70 baada ya kutiwa hatiani katika mashtaka nane yakiwemo ya uchochezi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com