Viongozi wanane wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wamepelekwa katika gereza la Segerea kutokana na kushindwa kulipa faini ya Sh350 milioni.
Ni baada ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwatia hatiani katika mashtaka 12 katika ya 13 yaliyokuwa yanawakabili na kutakiwa kulipa faini hiyo lakini wameshindwa.
Uamuzi wa kuwatia hatiani umetolewa leo Jumanne Machi 10, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi.
Social Plugin