Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MEYA WA MANISPAA YA IRINGA ALIYENG'OLEWA KUKABIDHI OFISI LEO


Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe amesema atakabidhi ofisi na gari la meya leo Jumanne asubuhi baada ya kukamilisha taratibu za kiofisi.

Kimbe ametoa ufafanuzi huo kwa waandishi wa habari waliofika ofisini kwake kutaka kujua kwanini anaendelea na kazi licha ya kuondolewa madarakani siku chache zilizopita.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Hamid Njovu amesema kanuni zinamtaka meya huyo kuondoka ofisini ndani ya siku 30 na hivyo anatakiwa kukabidhi ofisi na gari mara moja.

Akizungumzia malalamiko ya meya kuwa hakutendewa haki katika mchakato upigaji kura, Njovu amesema uamuzi wa madiwani wa CHADEMA kutoandika chochote kwenye karatasi ya kura ndicho kilichomuangusha.

Aidha, amewaondoa hofu wananchi kuwa kazi za meya zitafanywa na Naibu Meya, Joseph Lyata, na watendaji wake wataendelea kutoa huduma kama kawaida.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com