TCRA YAWATAKA WANANCHI KUACHA KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO MTANDAONI NA KUAZIMANA SIMU


Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog.
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amewataka wananchi kutumia mitandao ya Kijamii kwa manufaa ya kuchochea maendeleo badala ya kusambaza vitu vya hovyo na taarifa za uongo pamoja na kuacha tabia ya kuazimana simu za mkononi ili kujiepusha na athari vitendo vya uhalifu mtandaoni.

Mhandisi Mihayo ametoa rai hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga. 

Mhandisi Mihayo alisema kumekuwepo na tabia ya baadhi wananchi kutumia mitandao ya kijamii vibaya ikiwemo kusambaza habari za uongo ‘ Fake News’ zinazosababisha wananchi kuingiwa na hofu,mashaka na kukosa amani katika maisha yao.

“Tumieni mitandao ya kijamii kujiletea manufaa katika maisha yenu badala ya kutuma vitu vya hovyo mitandaoni. Usitume mtandaoni kitu kinachowaleta watu mashaka na hofu”,alisema Mihayo.

“Acheni tabia ya kuazimana simu za mkononi,mtakuja kufungwa jela pasipokujua kosa limetoka wapi kwani unayempatia simu yako hujui anaitumia kwa lengo gani.Watu wengine wanaazima simu yako waitumie kufanya uhalifu. Simu yako ikitumiwa na mtu mwingine halafu akafanya kosa sisi tutakutafuta wewe mwenye simu ndiyo maana tunasajili laini za simu kwa alama za vidole”,aliongeza Mhandisi Mihayo.

Mhandisi Mihayo aliwatahadharisha wanafunzi na jamii kwa ujumla kuachana na tabia ya kutumiana picha za utupu hata kama ni wapenzi kwani athari zake ni kubwa picha hizo zikivuja mtandaoni huku akielezea kuwa ni hatari kutumia Video Call Whatsapp ukiwa umevua nguo kwani kumbukumbu zinabaki mtandaoni.

Kwa upande wake Afisa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano kutoka TCRA, Walter Mariki alishauri watumiaji wa mitandao ya kijamii kubadilisha mara kwa mara nywila ‘ Password’ zao na kuepuka kuweka taarifa zao binafsi ikiwemo namba zao za simu kwani zinawapa nafasi kubwa watu wabaya kufanya vitendo vya uhalifu.

Aidha aliwataka wananchi kuwa makini wanapotumia simu zao kutuma fedha ili kuepuka kukosea lakini pia kujiepusha na vitendo vya utapeli vinavyofanywa na baadhi ya watu na kuhakikisha wanatoa taarifa kwa watoa huduma za mawasiliano na polisi pindi simu zao zinapoibiwa ama kupotea.

Naye Meneja wa Tigo mkoa wa Shinyanga Sadock Phares akisoma Hotuba ya Mkurugenzi wa Kanda ya Ziwa kutoka TIGO,Uthman Madati kwa niaba ya Umoja wa Makampuni ya Simu Tanzania (TAMNOA), alieleza changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni utapeli katika huduma za kifedha ambapo wateja wengi wamekuwa wakilalamika kutapeliwa kwa njia moja au nyingine.

“Kama mwakilishi wa Kampuni za mawasiliano tumetoa tahadhari ya changamoto hii katika mawasiliano ambazo wengi wamekuwa wakikutana nazo hasa katika utapeli.Njia mojawapo wa kupunguza ni kumsaidia mtumiaji kuelewa namna ya kuongeza umakini katika matumizi ya mawasiliano hasa huduma za kifedha”,alieleza.

“Watoa huduma tumeendelea kutoa elimu kwa umma na kuwasisitiza watumiaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu kuhakikisha wanafahamu chanzo cha maombi ya pesa kwa njia ya mtandao na kuhakiki watu wanaowatumia fedha kabla ya kutuma pesa ili kupunguza au kuzuia athari za utapeli”,aliongeza Phares.

Aliitaja changamoto nyingine ni kuwa Mteja kuwa na laini ya simu ambayo haikusajiliwa kwa jina lake na kutoa taarifa ya uongo au maelezo yasiyo sahihi wakati wa kusajili laini ya simu.
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Tigo mkoa wa Shinyanga Sadock Phares akimwakilisha Mkurugenzi wa Kanda ya Ziwa kutoka TIGO,Uthman Madati kwa niaba ya Umoja wa Makampuni ya Simu Tanzania (TAMNOA),akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano kutoka TCRA, Walter Mariki kutoka Makao Makuu ya TCRA akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga.
Wanafunzi wa Chuo cha VETA wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga. 
Wanafunzi wa Chuo cha VETA wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtumiaji Duniani (World Consumer Rights Day) Kanda ya Ziwa yaliyofanyika leo Machi 9,2020 katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa wa Shinyanga. 
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post