Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James akiweka jiwe la msingi katika jengo la nyumba ya katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga.
Na Mwandishi wa Malunde 1 blog
Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Kheri James amewataka vijana wa kitanzania hususani wanachama wa CCM) kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa corona uliogundulika katika nchi ya China unaoendelea kusambaa kwa kasi kubwa katika mataifa mbalimbali ambao umesababisha vifo vya watu wengi.
Akizungumza katika hafla ya kuweka jiwe la msingi katika nyumba ya Katibu wa Jumuia ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga (UVCCM) uliofanyika Machi 7,2020 katika eneo la Ushirika Manispaa ya Shinyanga.
Alisema ugonjwa wa Corona umekuwa tishio kwa mataifa mbalimbali hususani nchini China ambako uliripotiwa kwa mara ya kwanza mwaka huu kutokana na virusi vyake kusambaa kwa kasi katika mataifa mbalimbali barani Ulaya na kusababisha vifo kwa watu wengi.
“Tundelee kuchukua tahadhari kuhusiana na ugonjwa huu, serikali yetu kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na watoto, imekwishatoa maelekezo kuhusiana na namna bora ya kujikinga na ugonjwa huu, tuendelee kumuomba Mungu maambukizi yake yasiweze kuingia nchini kwetu”,alisema James.
James alifafanua kuwa bila ya kuwa na jamii yenye afya bora maendeleo hayawezi kupatikana hivyo ni budi elimu kwa vijana itolewe kuhusina na kujikinga na ungonjwa huo pamoja na magonjwa mengine ambayo ni hatari na yanasababisha kupunguza nguvu kazi ya kwa taifa.
Sambamba na hilo James aliwataka Wenyeviti wa UVCCM mikoa yote nchini kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa nyumba za makatibu kwa ngazi za mikoa na wilaya kabla ya mwezi Mei 2020 ili kutoa fursa ya kujiandaa na uchaguzi mkuu.
Katika hatua nyingine James aliwataka Viongozi wa UVCCM katika mikoa yote wasikubali kuwa madalali kwa watu wanaojipitisha katika majimbo na kata mbalimbali wanaotafuta kwa kuwa wao hawana mamlaka ya kuwachagua ama kupitisha majina yao.
“Wanaotaka nyadhifa ndani ya CCM wasubirie chama chetu kitakapotangaza muda wa kuanza kuchukua fomu ndipo watakaporuhusiwa kufanya kampeni kwa sasa ni mwiko kwa mwanachama yeyote kufanya kampeni za chini chini kutafuata uongozi kabla muda haujafika”alisema James.
Naye mwenyekiti wa Jumuia ya Umoja wa vijana mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge amesema nyumba hiyo itatumia shilingi milioni 35 hadi kukamilika kwake na kumshukuru Mwenyekiti wa UVCCM taifa,James kwa kuwachangia mifuko 80 ya saruji huku mbunge wa mkoa wa shinyanga Lucy mayenga akitoa mifuko 20 na kufikia jumla 100.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa aliwataka makatibu wa chama hicho kuhakikisha wanazilea jumuia zote za CCM ili kuzijengea uwezo katika utekelezaji wa majumu yake ya kila siku katika kujijenga chama.
“Toeni ushirikiano kwa jumuia hizi ili ziweze kufanya kazi vizuri kwani kuwepo kwao sisi cha chama tunapata fursa ya kuwaandaa viongozi wa baadae kwa kuwapa maelekezo mazuri kuhusiana na namna bora ya kujiendesha”,alisema Mlolwa.
Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la nyumba ya katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga iliyopo katika eneo la Ushirika Mjini Shinyanga.
Baadhi ya wanachama wa CCM wakimpokea Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa.
Baadhi ya wanachama wa CCM wakimpokea Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Umoja wa vijana mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akimwongoza Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James kuelekea eneo la uwekaji wa jiwe la msingi la nyumba ya katibu wa UVCCM mkoa wa shinyanga.
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa shinyanga wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James.
Social Plugin