Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UJENZI MRADI WA MAJI PONGWE -MUHEZA UMEFIKIA ASILIMIA 90

 MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akimueleza jambo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma Zainabu Vullu kulia wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo la Tanki la Maji litakalotoa maji eneo la Pongwe kupeleka wilayani  Muheza wakati wa ziara yako wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Uwasa Dkt Fungo Ally


 MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly katikati akisisitiza jambo kwa kamati hiyo
 MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Zainabu Vullu kulia ni mjumbe wa kamati hiyo wakati wakiingia kwenye mradi huo
 Sehemu ya wajumbe wa kamati hiyo wakitembelea maeneo mbalimbali katika mradi huo
 AFISA Uhusiano wa Tanga Uwasa Devota Mayala kushoto akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo wakati walipotembelea mradi huo

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma Zainabu Vullu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamati hiyo kutembelea mradi huo

Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akielezea mradi huo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma



MRADI wa Maji kutoka Pongwe Kitisa Jijini Tanga hadi wilaya ya Muheza umeelezwa kwamba umefikia asilimia 90 ya ukamilifu wake huku kazi chache zilizobakia ni kufunga pampu. 

Mradi huo utakapokamilika unaelezwa kwamba utakuwa mkombozi mkubwa kwa wilaya ya Muheza na maeneo ya jirani ambako mradi huo utapita kuelekea wilayani humo na hivyo kuondosha kero ya kutokupatikana huduma hiyo muhimu. 




Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma ilipotembelea mradi huo na kujionea namna ulivyotekelezwa huku wakiridhishwa na namna ulivyotekelezwa.




Alisema kwa sasa masharti ya mkandarasi na msambazaji wamekubaliana msambazaji azifunge pampu hizo ili ziweze kuwa na muda wa matazamio kuwa na uhakika kwa kipindi chote ambacho wamekubaliana. 

Aidha alisema kwa sababu pampu walizokubaliana ni kubwa na gharama kubwa ambazo gharama zake ni zaidi ya milioni 100 hivyo isipokuwa na muda wa matazamio ni hatari sana kwa uendelevu wa mradi. 




Mkurugenzi huyo alisema changamoto kubwa ilikuwa ni malipo na sasa yamepatikana kwa hiyo wanategemea mkandarasi anawasiliana na mzabuni wa pampu ili aweze kufikia kuzifunga hizo na mwishoni wa mwezi wanne katikati inaweza mradi ukawa umekamilika na maji kufika Muheza. 


“Tunaishukuru serikali wakati inaoingia madarakani walikuwa na ilani ambayo ilitarajia kufikisha huduma kwa wananchi katika mwaka 2017 walianzisha mradi huo kupeleke maji Muheza na kwa sababu hali ya Muheza ilikuwa mbaya siku nyingi”,Alisema.



“Kwani upatikanaji wake ni asilimia 35 kwa hiyo mradi huo baada ya ukamilifu wake utafanikisha kifikia asilimia 65 na kuna kazi ndogo za kufanyika ikiwemo kufumua miundombinu ya maji Muheza na ikikamilika itapelekea upatikana na maji kufikia asilimia 85 hadi 90”,Alisema.



Awali akizungumza wakati alipotembelea mradi wa Pongwe Mwenyekiti wa Kamati hiyo Zainabu Vullu alisema kwamba wao kama kamati wameridhishishwa na mradi huo na kwamba kama walivyoelezwa kwamba utawanufaisha wananchi. 
Alisema kamati zote kwenye kipindi hiki kabla ya bajeti inapita kwenye maeneo mbalimbali kuangalia miradi ambayo serikali imewekaza ili kuona maslahi na manufaa makubwa yatakayopatikana kwa wananchi. 

Alisema ziara yao ni moja ya kutimiza kanuniz za kibunge kuangalia jinsi gani serikali imewekeza na leo wameona jinsi serikali imewekeza wana tenki la lita laki saba ambalo litasaidia pia na vijiji jirani ili kuweza kunufaika na mradi huo . 

“Niseme kwamba sekta ya maji ni muhumu sana kwa maisha ya mtanzania na inatakiwa kumtua mwanamke ndoo kichwani aweze kufanya kazi nyengine za uzalishaji manufaa ya tenki hilo sio wananchi hata viwanda vitakapoanzishwa watapata maji kutoka hapo hapo”Alisema 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com