Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAMBO YA NJE DKT. DAMAS NDUMBARO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CUBA NCHINI


Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazugumzo na Balozi wa Cuba nchini Mhe. Prof. Lucas Domingo Hernandez Polledo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumo hayo viongozi hao wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika sekta ya afya nchini na Cuba imeiomba Tanzania kuiunga mkono katika mpango wake wa kugombea kiti katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Pamoja na mambo mengine walizungumzia kuhusu jinsi ya kuboresha mahusiano yaliyopo katika kati ya Tanzania na Cuba, ambapo Cuba imekuwa mdau muhimu wa maendeleo ya sekta ya afya nchini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com