Rais Magufuli amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya corona akisema ni hatari zaidi kwa maelezo kuwa ni ugonjwa hatari na Shirika la Afya Duniani (WHO) limeshatoa tahadhari.
Ametoa tahadhari hiyo leo Ijumaa Machi 13,2020 wakati akizindua karakana ya kisasa ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) iliyojengwa kwa Sh8.5 bilioni kwa ufadhili wa Serikali ya Ujerumani.
Rais Magufuli amesema ingawa ugonjwa huo umesambaa katika maeneo mbalimbali dunia bado Tanzania haujaingia.
==>>Hapo chini ni Kauli za Rais Magufuli Alizozitoa Leo kuhusu ugonjwa wa CORONA.
Kupitia hii hotuba yangu ya leo naomba tu watanzania wote mkachukue tahadhari kila mmoja kujikinga na ugonjwa wa Corona, upo na ni hatari unaua kwa haraka. Tanzania bara na Visiwani hakuna mgonjwa ila haina maana kwamba tusichukue tahadhari.
Niwaombe ndugu zangu tusipuuze ugonjwa huu. Kwa wale wanaopenda kusafiri safiri sana, kama safari sio ya lazima sana usisafiri. Nimeshatoa taarifa kwa Katibu Mkuu Kiongozi kwamba vibali vya kusafiri viwe kwa safari maalum
Tusishikane mikono, tusibusuane, sasa sifahamu usiku watafanyaje, lakini napo unaweza tu usibusu mambo yakawezekana na ni raha tu.
Na hii tahadhari msiwaachie viongozi tu ndio wazungumze,kila mmoja kwenye familia yetu tutoe elimu ya tahadhari. mashuleni walimu watoe tahadhari kwa watoto wetu, kwenye makambi etc ili tuweze kudhibiti hili gonjwa lisiweze kuingia nchini mwetu, gonjwa hili linaharibu uchumi wetu.
Niwaombe wahariri wa magazeti ikiwezekana kila siku kwenye gazeti watoe tahadhari ya ugonjwa wa Corona.
Kwenye Tv na redio zetu hata kabla ya kutangaza taarifa ya habari basi wapitishe mistari ya tahadhari ya ugonjwa huu.
Tukidharau ndugu zangu tutakwisha, mpaka sasa wanatibu tu symptoms lakini dawa ya kuponesha Corona haipo. Kupitia meseji hii ambayo naitolea hapa jeshini Lugalo ikawaguse watanzania.
Vyombo vya habari mkilisimamia hili tutashinda hii vita, unapopiga Muziki weka na tangazo la corona ili anaecheza na kubinuka amevaa kichupi anaweza akavaa hata gauni kwa kusikia tu neno corona, wekeni Dakika hata moja ya kuelimisha, Wanahabari hili ni jukumu lenu kubwa
Niwaombe viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali kila mmoja katika imani yake tuendelee kumuomba Mungu aweze kutusaidia, Mungu anaweza kila kitu.
Hata wakati wa Sodoma na Gomora tahadhari zilitolewa Watu walidharau wakaangamia, tahadhari tuzizingatie.
Nchi zimepunguza safari hata sisi Ndege yetu inayoenda India ilienda jana ikirudi leo haitoenda tena. Nchi yetu inaenda vizuri kiuchumi, janga hili litaturudisha nyuma.
Social Plugin