Wakati ugonjwa wa virusi vya corona ukiwa unaenea kwa kasi katika maeneo mbalimbali ulimwenguni,Waziri mkuu wa Rwanda Dkt.Ngirente ametoa maagizo 10 ya kukabiliana nao.
Baadhi ya maagizo aliyoyatoa Dkt.Ngirente ni pamoja na kutoruhusu safari zisizo za lazima,malipo ya kieletroniki zaidi yatatumika kuliko kutumia ATM ,Waajiriwa/Watumishi wote wa umma na sekta binafsi watafanya kazi wakiwa majumbani isipokuwa wale watoa huduma muhimu.
Maagizo mengine ni mipaka yote kufungwa,isipokuwa usafiri wa mizigo,safari kati ya miji na wilaya tofauti ndani ya nchi hairuhusiwi isipokuwa kwa sababu za matibabu,usafirishaji wa chakula au bidhaa muhimu zitaruhusiwa.
Pia Dkt.Ngirente ameagiza maduka na masoko yote kufungwa isipokuwa yale yanayouza chakula,Dawa, vifaa vya usafi huku baa zote zikifungwa.
Social Plugin