WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa lengo la
serikali kuhamisha baadhi ya makao makuu ya wilaya ni kusogeza huduma
karibu na wananchi.
Waziri
Mkuu alisema hayo katika mji wa Mkata wilayani Handeni baada kuzungumza
na wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela kutoa
ufafanuzi sababu za kuhamishia makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya
Handeni kuhamishiwa katika mji wa Mkata.
Shigella
alisema kuwa,makao makuu kuhamishiwa katika mji huo yamezingatia mambo
mengi ikiwemo kuangalia kusogeza huduma kwa wananchi.
"Kuhamishia
makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Handeni tumeangalia mambo mengi
tumeona kuwa wananchi kufuata huduma Mkata ni nafuu zaidi ambapo mtu
anatumia gharama ya shilingi kati ya 3,000 na 5,000 wakati ukienda
Kabuku unatumia shilingi 10,000,"alisema.
Alifafanunua
kuwa baada kuangalia hilo,baraza la madiwani la halmashauri
hiyo,walipiga kura kuona ni wapi panafaa kuwekwa makao makuu ambapo kati
ya madiwani 27 waliopiga kura,26 walipendekeza makao makuu yawe Mkata.
Akiwa
Kabuku,Waziri Mkuu alipata malalamiko kuwa makao makuu ya wilaya hiyo
yamehamishwa kibabe bila ya wananchi kushirikishwa na kutaka maelezo
kuujua ukweli.
Akitolea
ufafanuzi suala hilo,Waziri Mkuu amesema kuwa yeye hawezi kupinga
maamuzi ya Makao makuu kuwa Mkata ikiwa yamezingatia matakwa na sera ya
serikali ya kusogeza makao makuu karibu na wananchi.
Amesema
kuwa tayari serikali imeshatoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa
ajili ya ujenzi wa makao makuu ya wilaya na serikali itaendelea kutoa
fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi.
Sakata
la mgogoro wa mvutano wa kujua wapi kujengwe makao makuu ya wilaya kati
ya Mkata au Kabuku lilipelekea kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Halmashauri
ya Wilaya ya Handeni,Ramadhani Diliwa diwani wa Kata ya Mgambo kujiuzulu
nafasi yake mwaka 2018.
Social Plugin