Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Kiwanda cha
Tanga Cement cha Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya siku sita ambapo alitembelea kiwandani hapo kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa
kiwanda hicho Reinhardt Swart kulia ni Waziri wa Madini Dotto Biteko
Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mkurugenzi wa Mtendaji wa
kiwanda hicho Reinhardt Swart akizungumza wakati wa ziara hiyo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa ziara hiyo.
SERIKALI
imesema kuwa itaendelea kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na kuondoa
changamoto zote zinazokwamisha kwa namna moja au nyingine sekta ya uwekezaji
nchini.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo leo Jumanne
wakati alipotembelea kiwanda cha saruji cha Simba Cement cha jijini Tanga ambapo alifanya mazungumzo na
uongozi pamoja na wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Amesema kuwa,uzalishaji wa saruji nchini ni mkubwa kiasi
kwamba hawawezi kuagiza saruji nje ya nchi kwa kulinda viwanda vya ndani.
“Malengo ya serikali ni kufanya kazi pamoja na wawekezaji
kutokana uwekezaji huu una tija kwa serikali kutokana na kodi zinazolipwa na
wawekezaji zinasaidia katika kutekeleza kwenye miradi ya maendeleo tunayoiona na
kwa upande wa uzalishaji wa saruji tunajitosheleza,ndio maana hatuagizi saruji
nje,”alisema.
Aliongeza kwa upande wa changamoto zinazokikabili
kiwanda cha Simba Cement amesema atakutana na uongozi wa kiwanda hicho ofisini
kwake jijini Dodoma pamoja na mawaziri wenye dhamana za
Madini,Uwekezaji,Viwanda pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli
nchini(TRC) uongozi wa kiwanda hicho watoe mapendekezo yao ili waone ni kwa namna
gani waweze kuzitatua changamoto hizo.
“Machi 10 ninataka uongozi wa kiwanda cha saruji cha
Simba Cement tukutane Dodoma pamoja na Waziri wa madini,Nishati,Viwanda na
uwekezaji mlete mapendekezo yenu tuone ni namna gani tunaweza kutatua
changamoto zenu kutokana hiki ni moja ya kiwanda kinacholipa vizuri kodi pamoja
na kuwa na soko kubwa ndani na nje ya nchi,”alisema.
Alisema kuwa kuhusu changamoto ya usafiri iliyoikumba
kiwanda hicho,serikali imeagiza mabehewa 100 na kati ya hayo mabehewa 40
watayaleta katika kiwanda hicho ambacho mahitaji ya mabehewa kwa siku katika
kiwanda hicho ni 80 ili kupunguza changamoto ya usafirishaji wa saruji hiyo
katika maeneo mbalimbali nchini.
“serikali imeagiza mabehewa 100 kati ya hayo tutayaleta
Simba Cement ili kuondoa changamoto ya usafirishaji,hapa mahitaji ya mabehewa
kwa siku ni mabehewa 80,”alisema.
Aidha,kuhusu nishati ya umeme amefafanua kuwa serikali inatekeleza miradi ya ujenzi wa
miundombinu ya uzalishaji umeme nchini na muda si mrefu changamoto hiyo
itatatuliwa.
Kwa upande wake,Waziri wa Madini Dotto Biteko,alisema
kuwa kiwanda hicho ni moja ya viwanda ambavyo vimekidhi masharti na vigezo
vyote vya viwanda nchini hivyo kuhusu changamoto ya upatikanaji wa changamoto
ya makaa ya mawe wataitua.
Awali,Mkurugenzi wa Kiwanda cha Saruji cha Simba
Cement,Reinhardt Swart,alimuambia Waziri Mkuu kuwa hivi karibuni kiwanda hicho
kimekumbwa na changamoto ya nishati,usafirishaji ambapo uzalishaji ni mkubwa
lakini usafirishaji ni mdogo kutokana sehemu kubwa wanatumia usafiri wa treni
kusafirisha saruji lakini mabehewa yanayokuja ni kidogo ukilinganisha na
uzalishaji kuwa mkubwa.
Amesema kuwa kiwanda hicho ni muhimu kwa uchumi wan chi na
watu wa Tanga kutokana kimeajiri wafanyakazi 360 na kutoa ajira zisizo rasmi
600.
Social Plugin