Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa kama nchi haiwezi kuchukua tahadhari kama zilivyochukuliwa na Mataifa mengine duniani ya kupambana na Virusi vya Corona kwa kuwa watu wengi nchini maisha yao ni ya kubangaiza siku kwa siku.
Hayo ameyabainisha leo Machi 31, 2020, Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 Mkutano wa 19.
"Hatuwezi kuchukua measure za wazungu na kuzi copy na ku- paste hapa kwetu kama zilivyo, tutaua watu wetu, lazima tuangalie maisha yetu ya Kitanzania na kujaribu kuchukua hatua kufuatana na mazingira yetu" amesema Spika Ndugai.
Amesema katika maeneo yenye masoko wanatakiwa kuchukua hatua kadhaa kama kuweka maji ya kunawa na sabuni, kutokaa karibu ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
“Kuna nchi polisi wanapiga watu viboko ikilazimika huko Serikali itafanya lakini hatuishauri kwa sasa, tunajaribu kuelimisha zaidi, kutoa wito na kumuomba Mungu atuepushe na janga hili ambalo limezitikisa nchi zenye uchumi mkubwa,” amesema Ndugai
Social Plugin