Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza na wakati wa mkutano wake
na vyombo vya habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya maji inayoanza Machi
16 hadi 22 mwaka huu kulia ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi
Upendo Lugongo kulia akisistiza jambo wakati wa mkutano huo kushoto ni
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly
Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua matukio mbalimbali
Mwandishi wa Gazeti la Citizen Mkoa wa
Tanga George Sembony kushoto akiwa na Amina Omari wa gazeti la Mtanzania
wakifuatilia mkutano huo kwa umakini
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imewataka wateja wao kuchukua
tahadhari na kufuata maelekezo kama watakavyoongozwa wakati wakupatiwa huduma ikiwemo kuepuka
kurundikana kwa pamoja kwenye madirisha ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa
Corona.
Amesema tahadhari hiyo wameichukua ikiwa ni hatua
mojawapo kuunga mkono juhudi serikali kuzuia kuingia nchini ugonjwa huo kwa kutoa elimu kwa
njia ya jumbe mbalimbali katika maeneo ya ofisi zao,hususani majengo ya
huduma kwa wateja pamoja na kuwa na sehemu za wateja pamoja na watumishi
kuosha mikono yao
Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Mamlaka
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi
Geofrey Hilly wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari kuhusu
maadhimisho ya wiki ya maji inayoanza Machi 16 hadi 22 mwaka huu.
Alisema
kwamba kwa kuwa maeneo yao hususani kwenye ofisi za kutolea huduma ni
mojawapo wa maeneo yenye mwingilio mkubwa wa watu hivyo ni wajibu wao
kuhakikisha wanachukua tahadhari ya kukabiliana na ugonjwa huo.
“Kufuatia
na maagizo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa nchi juu ya ugonjwa
huo sisi kama mamlaka tumeona ni muhimu kuanza kuchukua hatua mapema za
kukabiliana nao”Alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema miongoni mwa
tahadhari ambazo zimeanza kuchukuliwa na mamlaka ni pamoja na kuunga
mkono serikali kwa kutoa elimu juu ya ugonjwa huo kwa njia ya ujumbe
mbalimbali katika maeneo ya ofisi ,majengo ya huduma kwa wateja kuwa na
sehemu za wateja na watumishi kwa ajili ya kuosha mikono.
“Sisi
tumekuwa na madirisha ya huduma kwa wateja hivyo ndio maana tumeamua
kuchukua tahadhari hivyo kutokana na kwamba wakati mwengine wateja
wanakuwa na fujo wanarundikana wanataka kila mmoja asikilize kwa wakati
na ndio maana tumeamua kufanya hivyo”Alisema
Mkurugenzi huyo
alisema kwamba wataweka huduma ya kunawa mikono kwa sababu ugonjwa huo
asilimia kubwa unatokana na kugusanagusana kwa hiyo kila wakati mtu
ahakikisha amenawa mikono na sabuni.
“Tunasisitiza kuchukua
tahadhari watumishi na wateja wote lakini pia tutaweka maeneo ya kunawa
mikono kwenye ofisi zao kuwasaidia watu ambao wanakuja kupata huduma
kunawa mikono “Alisema
Awali akizungumza wakati wa mkutano huo
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo alisema
upatikanaji wa maji vijijini kwa wastani ni asilimia 52 lakini kwenye
mikuu ya wilaya ni asilimia 54 na Jiji la Tanga ni asilimia 89 na watu
wanapata maji safi.
Alisema kwa Tanga wapo vizuri na
wanajitahidi miradi yote inakwenda kutekeleza kupitia njia ya uwezo wa
ndani na wakandarasi watatumika kwa uchache ili wananchi waweze kupata
huduma kwa haraka ndani ya muda mfupi.
Social Plugin