Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Ilala, Dk Milton Makongoro Mahanga amefariki dunia leo Jumatatu Machi 23, 2020katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katibu wa Chadema Kanda ya Pwani, Hemed Ally amesema wamepata taarifa za msiba huo.
“Ni kweli taarifa hizo tumezipata kupitia katibu wa Chadema wa Mkoa wa Ilala maana yeye ndiye alikuwa anafanya naye kazi kwa ukaribu,” amesema.
“Ilikuwa twende tukamuone leo na taarifa zote zilikuwa zinapitia kwa katibu wake wa mkoa wa Ilala wa chama, sasa asubuhi alipofanya mawasiliano na mke wake akamueleza kuwa Dk Makongoro amefariki dunia,” amesema.
Social Plugin