SHIRIKA
la Uwakala wa Meli Tanzania Mkoani Tanga (TASAC) limetoa wito kwa vyombo vya usafiri vinavyofanya kazi zake majini
ambayo havijakaguliwa na kupata cheti cha ubora kutokwenda majini
kufanya shughuli zake.
Agizo
hilo lilitolewa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani
Tanga Captain Christopher Shalua wakati akizungumza na mwandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema
kwamba wao wanatoa wito kwa vyombo vya majini kwa kipindi hiki cha masika
vyombo ambavyo havijakaguliwa na kupata cheti cha ubora haviruhisiwi kwenda
majini.
Afisa Mfawidhi huyo alisema pia kwa kipindi hicho vyombo vyote vilivyopata
vyeti vya ubora ni vizuri kuchukua tahadhari kuhakikisha vifaa vyote vya umuhimu
ikiwemo pampu za kutolea maji yaliyoingia kwenye chombo zinafanya kazi na zipo.
Aidha
alisema kwa vyombo ambavyo na vyombo havitakuwa
na vifaa vitakavyostahili kuruhusu kwenda majini wanavitaka visienda kufanya
shughuli zozote majini kwa kuchukua tahadhari.
“Tunatoa
rai kwa vyombo vizingatia maelelezo hayo kwa sababu kipindi cha masika
kinaambatana na hali mbaya ya hewa mawimbi makubwa pamoja na mvua ambazo
zinasababisha maji kuingia kwenye chombo na kusababisha uzito”Alisema
Alisema
kwamba hivyo kama uwezo wa kutoa maji kwenye chombo utakuwa ni mdogo itakuwa
rahisi kuzama na hivyo tunatoa wito kwa vyombo vyote hasa kwa
uvuvi maelekezo hayo yazingatiwe.
Hata
hivyo aliwataka watendaji wa serikali za vijiji na mitaa maeneo ya vyombo vya
uvuvi,mizigo vinapotoka kwenye maeneo yao vimekaguliwa na kupatiwa cheti cha ubora
na idadi ya vifaa vya uokozi maalumu baharini kulingana na idadi ya wafanyakazi
waliopo kwenye chombo hicho.
Social Plugin