Waziri wa ujenzi Mhandisi Isack Kamwelwe, naibu waziri, Elias Kwandikwa, mkuu wa mkoa wa Morogoro na viongozi wa wizara wamewasili katika eneo la Kiyegeya lilipokatika daraja kwa kazi ya kurudisha mawasiliano ya barabara kuu ya Dodoma - Morogoro.
Kazi ya matengenezo ya daraja hilo imeanza kwa kuweka vifusi na mawe huku madaraja mawili ya chuma yakiwa yanaunganishwa ili kufungwa kwenye eneo lilipokatika.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kuandikwa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inafanya matengenezo kwa haraka ili mawasiliano yaweze kuendelea kwani barabara hiyo inategemewa kiuchumi si kwa mikoa ya Kanda ya Kati na ziwa pekee bali hata nchi jirani za maziwa zikiwemo Uganda, Burundi, Congo.
Amesema muda si mrefu madaraja ya chuma yatafungwa eneo hilo ili kupitisha maji na baadaye waanze kuweka mawe ya kutosha ili mawasiliano yarejee.
Social Plugin