Kulia ni Waziri wa Nishati Dkt Medadi Kalemani.
Waziri wa Nishati Dkt Medadi Kalemani amemuagiza Mkurugenzi wa TANESCO kumchukulia hatua kali Msimamizi wa Kituo cha kupooza umeme cha Ubungo Mhandisi Abubakar Issa kwa kukata umeme Ijumaa Machi 20, 2020.
Dkt Kalemani pia ametoa onyo kwa mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kote nchini kuacha tabia ya kukata umeme na kufanya mgao kwa kisingizio cha mitambo ya kuzalisha Umeme kushindwa kufanya kazi.
Katika Hatua nyingine Waziri Dkt Medadi Kalemani amewataka wananchi wanaofanya shughuli zao kandokando mwa mto ambako maji ya bwawa la Mtera yanaelekea kuondoka ili kujinusuru na athari za maji yanayofunguliwa kutoka bwawa la Mtera.
Kufuatia zoezi la Kufunguliwa kwa Maji katika daraja la Mtera ili kupunguza ujazo wa maji katika Bwawa hilo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema tayari tahadhari imetolewa kwa wananchi ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.
Imeelezwa kuwa Ujazo wa Maji katika Bwawa la Mtera umefikia mita za ujazo 698.74 kiwango kinachostahili kwaajili ya Uzalishaji wa Umeme jambo ambalo limesababisha serikali kufungua na kupunguza ujazo huo katika bwawa hilo.
Chanzo - EATV
Social Plugin