Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WABUNIFU WATAKIWA KUBUNI KAZI ZA KUWAINGIZIA KIPATO ......PIA JAMII YASHAURIWA KUTUMIA MKAA MBADALA ILI KUTUNZA MAZINGIRA


Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Wabunifu wa kazi za Sanaa na ubunifu hapa nchini  wametakiwa kubuni kazi ambazo zitawaletea kipato na kuachana na bunifu za kujifurahisha ambazo haziwasaidii katika kupata kipato kwani bunifu ni muhimu kuelekea uchumi wa Viwanda.



Hayo yamebainishwa  Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa idira ya sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu Profesa Maulilio kipanyula, wakati wa ufunguzi wa semina ya washiriki katika wiki ya maonyesho ya bunifu zinazofanywa na watanzania, ambazo zitafanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Amesema ni muhimu wabunifu wote wakabuni vitu ambavyo vitawasaidia katika kupata kipato na sio kubuni bunifu za kujifurahisha ambazo haziwasaidii katika kupata kipato.

"Umefika wakati wabunifu wetu mbuni vitu ambavyo vitawasaidia kupata kipato msibuni vitu ambavyo haviwaletei maendeleo mjikite katika bunifu ambazo zitawasaidia kiuchumi" amesema Prof. Kipanyula.

Amesema lazima bunifu wanazobuni zinakuwa na mchango kwenye uchumi wa taifa hasa kipindi hiki tunaelekea katika uchumi wa Viwanda, kwa maendeleo ya nchi na mtu kipato Cha mtu mmoja mmoja.

Amebainisha kuwa ubunifu sio sayansi tu bali ni kila kitu ambacho unabuni ambacho kitasaidia katika kurahisisha vitu flani na upo kila mahala sio lazima uwe umesoma masomo ya sayansi.

"Ubunifu sio mpaka uwe umesoma Biology, sijui hisabati, Physics hapana ubunifu ni mahala popote ambapo unaweza kubuni kwa kujiongeza na kitu kikawa na msaada kwa kurahisisha kitu flani au mahitaji ya soko" amesema.

Amesema ni muhimu kutumia teknolojia za ndani kuliko kutegemea teknolojia za nje ambazo hazitatusaidia kama nchi, ni muhimu kukuza bunifu za ndani, na kuahidi kuziendeleza bunifu hizo na Wizara itahakikisha bunifu zote zinatambuliwa zinasimamiwa na zinasaidiwa ili ziwe na mchango katika Jamii.

Amesema makundi ya wabunifu yatakayoshiriki ni makundi Saba (7) ambayo ni shule za msingi, shule za Sekondari, vyuo vya ufundi, vyuo vya ufundi wa kati, vyuo vikuu, taasisi za utafiti na maendeleo na wabunifu kutoka sekta isiyo rasmi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Capital Space, ambayo huwalea wabunifu, bw. Abdallah Mbwana, amesema taasisi hiyo huwasaidia wabunifu na wajasiliamali katika kutengeneza mifumo ya bunifu zao kuwa biashara.

 Naye Mkurugenzi  wa kampuni ya Kuja na Kushoka  inayotengeneza mkaa  mbadala ,Leonard Kushoka  akizungumza na wanahabari katika maonesho hayo ya MAKISATU  ametoa wito kwa jamii kuacha  kuharibu Mazingira mazingira kwa kukata miti  ovyo badala yake watumie mkaa mbadala kwa kutumia takataka  na mabaki ya mimea  yanayozalishwa majumbani kila siku.

 Kushoka amebainisha  kuwa,kumekuwepo na uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kukata miti hoyo  kwa mahitaji ya mkaa lakini kiwanda chake kimekuja kutatua tatizo la ukataji miti hovyo kwa kuwalete mashine ya mkaa mbadala na kwa bei nafuu.

Amesema kwa mkaa huo sio lazima utengenezwe kwa mashine , kuna uwezekano mkubwa kwa mtu kutengeneza mkaa huo hata akiwa nyumbani  kwani teknolojia hiyo ni raisi kutengenezeka .

“ Takwimu kutoka TFS zinaonyesha kuwa karibu hekta 4000 hualibika kila mwaka kutokana na ukataji wa miti kutokana na mahitaji ya mkaa katika jamii hivyo kutokana na changamoyo hiyo tukaona ni vyema tuje na huu mpango wa kutengeneza mashine ya mkaa mbadala, ”alisema Mkurugenzi huyo Kushoka.

Aidha amesema kuwa,Kampuni yao pia inatengeneza ajira kwa vijana kwani mpaka sasa wameshasambaza mashine 30 kwa vijana lengo ni kusambaza mashine hizo za kutengeneza mkaa mbadala kwa vijana 100 ambapo hapo tutakuwa tumetengeneza ajira kwa vijana 150.

Ameiomba serikali kuwekeza kwa nguvu kubwa kwenye teknolojia hiyo na ikiwezekana kila kwenye kata kuwepo na mashine moja ya kutengenezea mkaa kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuondoa tatizo la kuzagaa kwa takataka katika miji ambazo zinatumia fedha nyingi katika kuziteketeza.

“ Kama jiji la Dar es sallam linauwezo wa kutumia mkaa wa bilioni 2 basi serikali ikiwekeza katika mashine hizi tutapunguza ukataji miti na uharibifu wamazingira  kwani kila  kilo moja ya mkaa mbadala inatengeneza kilonne ya mkaa wa miti,”alisema Kushoka.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com