Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WATISHIA KUFUNGA MNARA WA SIMU ZA MKONONI KWA KUDAI KODI YA PANGO

SALVATORY NTANDU

Serikali ya kijiji cha Bunango kata ya Bugarama Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imeitaka kampuni ya Helious Tower Tanzania inayosimamia minara ya Mawasiliano ya simu za mkononi kuleta majina ya madalali wanaolipwa fedha za kodi ya pango la minara iliopo katika kijiji hicho baada ya kufanya uhakiki na kujiridhisha kuwa si wamiliki halali wa maeneo yaliyojengwa minara hiyo.

Uamuzi huo umetolewa Machi 23 mwaka huu na Mwenyekiti wa kijiji cha Bunango Anna Peter kata ya Bugarama katika Halmashauri ya Msalala wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wanaomiki maeneo yaliyojengwa minara hiyo kuhusiana na kutolipwa kodi zao za pango.

Alisema kuwa baada ya kupokea Malalamiko hayo walikaa na kufanya uhakiki juu ya umikili wa maeneo hayo ambapo walibaini kuwepo kwa madalali waliofunga mikataba na kampuni za mawasiliano kinyemela na kulipwa kodi za pango kila mwaka huku wamiliki halali wakiachwa bila kupewa kitu chochote.

“Katika eneo la Mzee Robert Busengwa limejengwa minara miwili ya Kampuni za Airtel na Vodacom sisi kama serikali ya kijiji tumebaini katika eneo ulipojengwa manara wa Vodacom kunadalali ambaye amefunga mkataba na kampuni hii na kulipwa kodi ya pango kila mwaka zaidi ya shilingi milioni 5.5 huku mmiliki halali akiendelea kuteseka”alisema Peter.

Amefafanua kuwa kisheria wamiliki wote wa maeneo yenye uwekezaji wa minara wanapaswa kulipa asilimia 20 ya mapato yao kwenye serikali ya kijiji lakini tangu minara hii imejengwa mwaka 2001 haijawai kulipa fedha zozote kwaajili ya maendeleo ya kijiji.

stahiki zangu naiomba Serikali seikivu ya Rais  Dk John Pombe Magufuli inisaidie mimi mnyonge ili nipate haki zangu,nimechoka kuzunguka nimetumia fedha nyingi ila msaada hakuna,”alisema Busengwa.

Akijibu Malalamiko ya Wakazi hao Msimamizi mkuu wa Minara ya Mawasiliano kutoka kampuni ya Helious Tower mkoa wa Shinyanga ambaye hakutaka jina lake litajwe Gazetini kwa madai kuwa si msemaji wa kampuni hiyo aliwataka wananchi hao kuandikika malalamiko yao na kuyapeleka makao makuu jijini Dar es salaam ili waweze kupata haki zao.

“Haiwezekani mnara ujengwe hapa kwa zaidi ya miaka 10 na kodi ya pango inalipwa kila mwezi halafu asijulikane anayelipwa Helious Tanzania inalipa kodi kila mwaka za upangaji andikeni malalamiko yenu kwa maandishi myatume Makao makuu yatafanyiwa kazi,”alisema.

Mwisho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com