India imewanyonga hadi kufa wanaume wanne walioshitakiwa kwa kosa la kumbaka na kumuua mwanafunzi mmoja ndani ya basi mnamo mwaka 2012.
Mwanamke huyo aliyekuwa na miaka 23 alibakwa wakati basi lilipokuwa likiendelea na safari mjini New Delhi.
Watu hao wamenyongwa mapema hii leo katika gereza la Tohar Jail mjini New Delhi hii ikiwa ni kulingana na shirika kubwa la habari nchini humo la Press Trust of India, lililonukuu mamlaka za gereza.
Wanaume hao walimbaka mwanamke huyo aliyekuwa akitokea kutazama sinema na kumuumiza vibaya kwenye sehemu zake za siri kwa kutumia kipande cha chuma.
Tukio hilo baya kabisa liliibua maandamano kote nchini India na kuwachochea wabunge kuongeza ukali wa adhabu dhidi ya kesi za unyanyasaji wa kingono.
Adhabu ya mwisho ya kunyongwa ilitolewa mwaka 2013 nchini India.
-DW
Social Plugin