Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATU WAWILI WAFARIKI KWA KUSOMBWA NA MAFURIKO YA MAJI MOROGORO


Watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha huku mmoja akijeruhiwa kufuatia mvua kumbwa zilizonyesha usiku wa kuamkia leo Manispaa ya Morogoro, baada ya Daraja lililopo Mtaa wa Kihimbwa Kata ya Boma  kuziba na kusababisha maji kupita juu ya Daraja.


Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kata ya Kihimbiwa Antipasi Kinange ambapo amesema mvua hiyo imeanza kunyesha usiku wa kuamkia leo na watu hao  walienda dukani kwa ajili ya kununua bidhaa ndipo maji yalipozidi na kusombwa na maji.

Waliofariki katika mvua hiyo ni mwanamke aliyefahamika kwa jina la Habia Sanga huku mwanaume akifahamika kwa jina moja la Salum.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com