WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Magamba Kata ya Magamba wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko akizungumza wakati wa ziara hiyo
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko akizungumza wakati wa ziara hiyo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa ziara hiyo
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesitisha zoezi la
uchimbaji wa madini ya Boxite katika mgodi uliopo Kata ya Magamba
wilayani Lushoto.
Pia,amemuagiza
Waziri wa Madini Dotto Biteko kuzichukua leseni zote 22 za wachimbaji
wakubwa na wadogo zilizotolewa katika mgodi huo.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo wakati alipoutembelea mgodi huo katika ziara yake wilayani Lushoto.
Amesema
kuwa,serikali ilipokea malalamiko ya wananchi kuhusu athari uchimbaji
madini katika mgodi huo zikiwemo uharibifu wa mazingira na athari za
kiafya.
Pia amesema
kutokana na uzito wa mgogoro uliobuka katika mgodi huo,Rais mstaafu wa
Serikali ya Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa alimuagiza kufuatilia wakati
wakiwa Msumbiji kwenye hafla ya kuapishwa Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi
kuwa atembelee wilayani Lushoto kusikiliza kilio cha wananchi na atoe
tamko la serikali.
Amesema kuwa serikali imefanya maamuzi hayo kutokana inasikiliza wananchi wake kutoka na hoja zao walizozitoa.
"
Serikali imefanya maamuzi,imesitisha kila kitu baada ya kusikiliza
maoni ya wananchi kuhusu kero na athari za afya zinazotokana na
uchimbaji huo,"alisema.
Aliongeza,
"Waziri wa Madini chukua leseni zote 22 za uchimbaji madini
zilizotolewa eneo hilo na wananchi lindeni eneo hilo wasiingie watu
kuchimba,"alisema.
Kwa
upande wake,Waziri Biteko alisema kuwa mgogoro huo wa kuzuia uchimbaji
katika mgodi huo ulianza muda mrefu lakini mwezi August 30,mwaka jana
walifanya mkutano mkubwa na wananchi na kutoa malalamiko mengi ikiwemo
athari zinazotokana na uchimbaji huo.
Alifafanua
kuwa baada ya kusikiliza maoni hayo,September 4,mwaka jana waliandika
barua wa wachimbaji wote kusitisha zoezi la uchimbaji katika mgodi huo.
Mbunge
wa jimbo la Lushoto Shabani Shekilindi alisema kuwa eneo hilo ndio
chanzo kikubwa cha maji katika maeneo mbalimbali katika jimbo hilo,hivyo
uchimbaji huo una athari kubwa za kiafya na kimazingira.