Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu amaeahidi kupeleka Wataalamu wa mazingira kwa ajiili ya kufanya tathmini katika eneo la Kwamgogo lililopo Kisiwani Pemba ambalo limeathirika na mabadiliko ya tabianchi. Amesema hayo kisiwani Pemba alipotembelea eneo hilo kujionea athari za kimazingira zilizosababishwa na mabadiliko ya tabinchi.
Ameongeza kuwa lazima jitihada za haraka zichukuliwe katika eneno hilo ili kuweza kuepusha kisiwa cha Pemba kisiharibiwe na mabadiliko ya tabianchi. “ tutaleta Watu wafanye tahtmini ni kitu gani tufanye ili kuzui haya maji kuja tena au kuyazuia yarudi huko yalikotoka na kuweza kunusuru eneno hili”alisema Waziri Zungu
Kijiji cha Kwamgogo kimeathirika na mabadiliko ya tabianchi kwa kusababisha maji kujaa na kuharibu mazingira ikiwemo kusababisha Wananchi kukosa njia ya kupita wakati wanaenda sokoni au kwenye shughuli zao za kila siku hivyo kusababisha Wananchi kuvuka kwa kuogelea kwenda ng’ambo ya pili kwenye huduma muhimu za kijamii.
Amewashukuru pia Wananchi wa Mkoa huo na Uongozi wa Mkoa kwa kuweza kuchukua hatua kwa kupanda mikoko na ili kuweza kupunguza athari hizo za kimazingira katika kijiji hiko cha Kwamgogo.
“Namshukuru saana Mkuu wa Mkoa pamoja na Wananchi wa eneo hili kwa jitihada mlizofanya kulinda mazingira katika eneo hili” alisema Zungu
Ziara hiyo ya Mheshimiwa Zungu ni maagizo aliyopewa na Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi baada ya kumtembelea Ofisini kwake kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira.